DC Farida Mgomi: Vitendo vya ukatili wa Kijinsia vinarudisha nyuma Ustawi wa Jamii na Uchumi wa Taifa

DC Farida Mgomi: Vitendo vya ukatili wa Kijinsia vinarudisha nyuma Ustawi wa Jamii na Uchumi wa Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi amewaasa wananchi wa Wilaya ya Ileje kuungana na kushirikiana kwa pamoja kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, kwa kukemea na kushirikiana na Vyombo vya Dola kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha jamii inabaki salama dhidi ya vitendo hivyo.

Akizungumza mapema Disemba 10, 2024 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Wilayani hapo akimuwakilisha Daniel Chongolo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe kama Mgeni rasmi, DC Mgomi ametoa wito kwa Wananchi kubadilika na kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani vinarudisha nyuma Ustawi wa jamii na kuzorotesha uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Aidha amewasihi wazazi kuwalinda Watoto kwa kuwapa malezi stahiki yanayozingatia maadili ya Kitanzania ili kuwaepusha watoto kuiga Tamaduni za nje ambazo zinakiuka miiko ya maadili ya Nchi yetu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameziasa familia kudumisha Upendo na kuepuka Migogoro sambamba na kutumia fursa zilizopo katika wilaya hii ili kujiongezea kipato kitakachowasaidia kutunza na kulea familia.

Sanjari na hilo Mgomi ametoa rai kwa Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia kuendelea kushirikiana na wananchi kwa kutoa elimu kuhusu Ukatili wa kijinsia sambamba na kuchukua hatua stahiki kwa wale wole watakaokutwa na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
 
Back
Top Bottom