DC Hai awashughulikia waliotafuna Sh126 milioni za Saccos

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
DC Hai awashughulikia waliotafuna Sh126 milioni za Saccos
Kwa ufupi
Mkuu wa Wilaya ya Hai amewataka watendani waliohusika na upotevu wa fedha hizo
kuzirejesha kwa wananchama haraka iwezekanavyo.

TUESDAY NOVEMBER 20 2018
By Janeth Joseph, Mwananchi
jjoseph@mwananchi.co.tz

Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka viongozi wa saba wa Saccos ya Uswaa Mamba iliyopo wilayani hapa kurudisha Sh126 milioni anazodaiwa kuzitafuna.
Wanaotuhumiwa ni karani wa Saccos hiyo, Jema Mwakatobe na wengine ni Godbless Uroki, Hellen Mtui, Salatiel Kweka, Godwin Kimaro, Japhet Shoo na Grace Massawe.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Uswaa kilichopo Machame, Ole Sabaya aliwataka viongozi hao kurejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo na ndani ya siku tatu wamueleze zilipo fedha hizo. "Staki blaa blaa hapa. Hizi fedha mmezichukua mafichoni na mtazirejesha hadharani, Serikali hii ni ya kutetea wanyonge, hatupendi kuona wananchi wakiteseka," amesema Ole Sabaya. Aidha amemuagiza, kaimu ofisa ushirika wa wilaya hiyo, Joel Marandu kufuatilia mwenendo wa chama hicho kujua kama kinawanufaisha wananchi.
Marandu amesema tangu alipopata malalamiko ya wananchi kuhusu upotevu wa fedha zao alianza kufuatilia. "Maagizo niliyopewa nitayafuatilia na kuyafanyia kazi" amesema Marandu.Karani wa chama hicho, Jema Mwakatobe alipohojiwa kuhusu
ubadhirifu wa fedha hizo amesema alikuwa akifuata maelekezo ya wajumbe wa bodi. "Nilipoingia kwenye chama hiki, nilikuwa bado mdogo, sikujua kinachoendelea hivyo nilikuwa naamriwa kusaini," amesema Mwakatobe.

Source:DC Hai awashughulikia waliotafuna Sh126 milioni za Saccos
 
Kuna SACCOS moja somewhere sitaki kuitaja mahali ilipo, kwa tetesi nilizokuwa nazipata kutoka kwa Mwenyekiti wake miaka kadhaa nyuma, kuna kipindi hadi BoT iliwahi kuidhinisha SACCOS hiyo iwe Benki, lakini hadi leo haijaweza kuwa, migogoro kibao na pesa hiyo ya kuanzisha Benki kama ipo tena! Hii nchi kazi kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…