DC Handeni apiga marufuku wanandoa kusoma meseji za wenzi wao

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe amelazimika kupiga marufuku Wanandoa wa Wilaya hiyo kuacha kusoma msg kwenye simu za wenzao ili kuepusha migogoro na vifo vitokanavyo na wivu wa kimapenzi, ameyasema haya kwenye maziko ya Kijana wa miaka 35 aliyeuwawa kwa kukatwa mapanga na kuchomwa visu kutokana na wivu wa mapenzi.

Wazazi wa Kijana huyu wamesema Mtoto wao ni kweli alishawahi kufumaniwa na Mwanamke wa Mtu lakini baadae alimlipa Mume wa Mwanamke huyo shilingi laki sita ili asamehe tukio hilo lakini sasa imewashangaza Mtoto wao kuuwawa kinyama.

Mama mzazi wa Marehemu amesema Mwanamke huyo alimwambia Mtoto wake kuwa hana Mume na hata baada ya kufumaniwa Mwanamke huyo aliendelea kumfatafata Marehemu

"Nilimwambia sikutaki wewe Mtoto lakini bado anakuja, anamletea Mwanangu majanga, naomba Serikali inisaidie waliomuua Mwanangu" β€”β€”β€” amesema Mama wa Marehemu.

Your browser is not able to display this video.
 
Ni kweli. Lakini ametimiza kauli tu mana ni ngumu kujuwa kama agizo linatekelezwa. Haya yote hutoa kwa wivu wa kupitiliza.

Moyo hauwezi kuuma kama hujasikia au hujaona. Nakumbuka katazo la waume kutonyonya maziwa ya wake zao ngumu. Mana huwezi kuingilia faragha zao.
 


Hapo hakutakuwa na u-serious na commitments kwenye huo uhusiano!
 
Tukiwaambia wadau humu waache wake za watu,, wanatuona kama sisi kwaya masters..... Wanaendelea kuimba nje ya sauti..

Huu ujinga unaoitwa Mapenzi una ushetani ndani yake,, na kijana ukiendekeza kibolodinda hakika yatakuua....

Kiukweli papuchi zilizo free ni nyingi,, Yanini ukaweke foleni kwenye papuchi ya mwenzako???,, kwanini tunategeana??? hizi zilizobaki azichakate nani..???

Ok, acha inyeshe..........
 
Tukiishi humu hakika ndoa zetu zitaimarika sanaa
 
Kuna mwamba kajitupia baharini huko lindi.. ITV habari.
Kaona isiwe tabu mwanamke alikuwa anamgomea. Tragic incident..πŸ˜ͺπŸ˜ͺ😭πŸ˜ͺ😭
 
Na hili nalo mkalitazame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…