Bakwata wanasema kuwa ni "mwanamke Muislam " kwa sababu mamlaka yao ipo kwenye Muislam. Tamwa na ndugu zake wao walipaswa kutetea mwanamke na CCM walipaswa kumtetea kama Mwana CCM.
Hapa kinachoonekana ni nani hodari wa propaganda tu.
Historia iliyowekwa kwanza licha ya kukosa ushahidi, haimaanishi kuwa kuvuliwa mtandio uliokwenda na nguo za kujistiri zisizobana sio vazi lililoamriwa kwa Waislam na pale Bi. Fatuma ameliwakilisha kuliko Waislam wengine au wenyewe.
Nafsi yangu ninawajua wanawake wengi walioolewa na Wakristo wakaendelea na dini zao na walipofika utuuzimani wakashika dini zaidi na kuvaa kama dini zao zinavyotaka ambapo hatua kubwa wanayofanya pia ni kujitenga makazi kimakazi na waume zao.
Kwa la huyu mama sijui, ila shamba la mumewe kufuga nguruwe au kuwa aliolewa na mkiristo hakumuondolei dini yake kama anayo. Naamini hakuna binaadamu aso dhambi kwa mujibu wa maamrisho ya dini afuatayo na angeamua kukaa chini angepata mengi ya kutafakari na kujutua
Pili hatujui Kama aliwathibitishia Bakwata kuwa yeye ni Muislam au la. Kwa vile Bakwata ni culprit wazoefu basi tunataka sana tuone na kwa hili pia waliokosea.Tunataka sasa atoe tamko rasmi kusema yeye ni Muislam. Kwangu huo nauona ni udhalilishaji wa aina nyengine kuwa sasa mtu alazimike kusimama mbele ya umma kulinda Imani yake!
Nadhani kimsingi hoja yako ingesimama vyema iwapo Bi Fatuma si Muislam na angesimama kupinga na kusema "yeye si Muislam" ili Bakwata iache kumtetea. Na ikiwa yeye ni Muislam hakuna lazima yoyote ya kusema hivyo kwa vile haki Yake tayari anaipata.
Sishabikii Bakwata kufikia kutoa matamko makali kiasi hiki, lkn haki ya kufanya hivyo wanayo kwa vile wanaemtetea anawakilisha Uislam.
Chadema did wrong kumvua mtu stara yake ambayo bila ya hiyo mwanamke Yule haamini kuwa kastirika. Purukushani ingetokea na wakamchanua blouse yake jee? Wangemtoa hivyo hivyo au wangemstiri? Ukosefu wa tact wameshindwa kuelewa kuwa mtandio na blouse una hadhi sawa kwa baadhi ya watumiaji. Na ikiwa jibu ni kuwa hata Kama angevuka blouse wangemtoa hivyo hivyo, I got nothing but to shake my head
(now hizi propaganda za JF aside mpaka zitakapoandikwa walau kwenye gazeti manake hapa mtu can say anything wala haombwi ushahidi na tunaamini kwa vile tu ni yenye kutupendeza)