Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amepongeza na kuyataja mashindano ya Mpira wa Miguu katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Babutale kuwa yamekuwa chachu ya hamasa kwa wananchi wakati wa zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililofanyika Oktoba 11 - 20, 2024.
DC Kilakala ametoa pongezi hizo Novemba 2, 2024 katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki muda mfupi baada ya kuanza Kwa mechi ya fainali ya kombe la mashindano hayo yaliyopewa jina la Samia Cup.
Mchezo wa fainali hizo umechezwa katika viwanja vya Ngerengere kati ya Kiroka FC na Matuli FC.