Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
DC KILAKALA: UKUSANYAJI WA MAPATO KUSAIDIA MOROGORO KUWA JIJI
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Musa Kilakala amesema kuwa Manispaa ya Morogoro haiwezi kufanikiwa kuwa jiji pasipo na mipango thabiti ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo vyake vya kodi.
Ameeleza hayo wakati wa kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya - DCC kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
DC Kilakala amesema kuwa moja ya mipango waliyonayo ni kufunga mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa mapato katika kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu mfumo ambao utafanana na ule wa Stendi ya Magufuli Mbezi jijini Dar es Salaam hatua hiyo inalenga kuhakikisha mapato yote yanakusanywa ipasavyo na kuzuia upotevu wa fedha.