Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti ametoa maelekezo ya kusimamishwa kwa mchakato wa utafutaji madini kwa kulipua mawe kwa baruti eneo la King’azi A kusimamishwa kwa kuwa hana vibali na hivyo anahatarisha usalama wa mali na Watu.
Kusoma hoja ya Mdau, bofya hapa ~ Jamaa anapasua mawe kwa baruti King'azi A (Kisarawe), maisha ya Watoto na nyumba yapo hatarini
Amechukua uamuzi huo baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai Wananchi wa maeneo hayo wamejaribu kumzuia mara kadhaa lakini ikashindikana na kuwa maisha yao pamoja na makazi yao yapo hatarini kwa kuwa mhusika amekuwa hazingatii usalama.
Akizungumza na JamiiForums, Magoti amesema “Maafisa wamewenda na wamekuta Mtu huyo anachimba madini, anatumia baruti na hana kibali, tulikuwa tunaweza utaratibu wa jinsi gani wachimbaji wa Madini Ujenzi wanaweza kufuata taratibu lakini huyo mtu akawa anaendelea.”
Ameongeza “Amechukuliwa kuwenda Polisi kutoa maelezo, unapotumia baruti unatakiwa kutoa taarifa kamili kwa Mamlaka kadhaa pamoja na Wananchi wanaozunguka, taarifa nilizopewa pia hata uchumbaji wake ni hatarishi, eneo limekaa kama kichuguu na linaweza kuanguka.”