DC Kiteto aeleza sababu nne zinazopelekea migogoro, adai 'kutokuheshimu Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ni chanzo kikuu'

DC Kiteto aeleza sababu nne zinazopelekea migogoro, adai 'kutokuheshimu Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ni chanzo kikuu'

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Katika kipindi kirefu kwa nyakati tofauti kupitia vyombo vya habari ikiwemo jukwaaa la JamiiForums.com zimekuwa zikiripotiwa taarifa za uwepo wa migogoro ya aridhi katika Wilaya ya Kiteto iliyopo Mkoa wa Manyara.

Hata hivyo kutokana na migogoro hiyo zimekuwa zikiripotiwa sintofahamu mbalimbali hasi ambazo uhusihanishwa na migogoro hiyo.

Katika kufahamu kinagaubaga kutoka kwa mamlaka ambazo zimepewa dhamana ya kuongoza Wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya Remidius Mwema anaeleza baadhi ya sababu ambazo zimekuwa zikichangia uwepo wa migogoro licha ya jitihada mbalimbali ambazo wanaendelea kuchukua katika kuleta suluhu.
IMG_1140.jpeg

Sababu nne ambazo zinabainishwa wazi na DC kuwa zimekuwa zikipelekea uwepo wa Migogoro katika Wilaya ya Kiteto.

Uvamizi wa Ardhi bila Kuzingatia taratibu za kisheria

Mkuu wa Wilaya Remidius Mwema anaeleza kwamba katika ufuatiliaji ambao amekuwa akiufanya akiwa pamoja na watendaji wengine kutokea Wilaya hiyo, amebaini kuwepo kwa wavamizi kuvamia maeneo yasiyo rasmi ikiwemo maeneo ya Hifadhi ya Jamii ya WMA na kuendesha shughuli mbalimbali haswa za Kilimo kinyume na utaratibu.

"𝙲𝚑𝚊𝚗𝚐𝚊𝚖𝚘𝚝𝚘 𝚒𝚗𝚊𝚢𝚘𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚢𝚊 𝙺𝚒𝚝𝚎𝚝𝚘 𝚗𝚒 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚔𝚞𝚗𝚊𝚔𝚞𝚠𝚎𝚙𝚘 𝚗𝚊 𝚞𝚟𝚊𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚗𝚊 𝚑𝚞𝚘 𝚞𝚟𝚊𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚗𝚒 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚒𝚗𝚐𝚒𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘, 𝚔𝚠𝚊 𝚖𝚏𝚊𝚗𝚘 𝚞𝚔𝚒𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚗𝚢𝚊𝚗𝚍𝚊 𝚢𝚊 𝚖𝚊𝚛𝚒𝚜𝚑𝚘 𝚢𝚊 𝙰𝚕𝚘𝚕𝚎 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 K𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚔𝚒𝚗𝚊𝚒𝚝𝚠𝚊 𝙰𝚖𝚎𝚒, 𝚞𝚟𝚊𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚞𝚖𝚎𝚏𝚊𝚗𝚢𝚒𝚔𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚝𝚊𝚔𝚛𝚒𝚋𝚊𝚗𝚒 𝚎𝚔𝚎𝚛𝚒 𝟻𝟶𝟶, 𝚆𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚟𝚊𝚖𝚒𝚊 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚏𝚢𝚎𝚔𝚊 𝚔𝚊𝚋𝚒𝚜𝚊 𝚖𝚒𝚝𝚒 𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚊𝚗𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘."anasema

"U𝚝𝚊𝚔𝚞𝚝𝚊 𝚖𝚔𝚞𝚕𝚒𝚖𝚊 𝚊𝚖𝚎𝚟𝚊𝚖𝚒𝚊 𝚑𝚒𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚊𝚞 𝚊𝚖𝚎𝚟𝚊𝚖𝚒𝚊 𝚗𝚢𝚊𝚗𝚍𝚊 𝚢𝚊 𝚖𝚊𝚛𝚒𝚜𝚑𝚘 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚠𝚊𝚔𝚊𝚝𝚒 𝚑𝚞𝚘 𝚑𝚞𝚘 𝚖𝚏𝚞𝚐𝚊𝚓𝚒 𝚊𝚗𝚊𝚊𝚖𝚒𝚗𝚒 𝚑𝚒𝚕𝚘 𝚗𝚒 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚕𝚊𝚔𝚎 𝚔𝚒𝚜𝚑𝚎𝚛𝚒𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚖𝚊𝚛𝚒𝚜𝚑𝚘, 𝚔𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚊𝚗𝚊𝚙𝚘𝚒𝚗𝚐𝚒𝚣𝚊 𝚖𝚒𝚏𝚞𝚐𝚘 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚕𝚊𝚔𝚎 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚜𝚑𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚕𝚒𝚙𝚘 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚑𝚒𝚕𝚘 𝚖𝚒𝚏𝚞𝚐𝚘 𝚒𝚔𝚊𝚒𝚗𝚐𝚒𝚊 𝚑𝚊𝚙𝚘 𝚖𝚘𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘 𝚗𝚍𝚒𝚙𝚘 𝚒𝚗𝚊𝚙𝚘𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚑𝚊𝚕𝚒 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚒𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚒𝚔𝚒𝚓𝚒𝚝𝚘𝚔𝚎𝚣𝚊

Anaeleza kwamba uvamizi umekuwa ukifanywa zaidi na watu kutoka nje ya Wilaya hiyo, ambapo anadai kwamba licha ya kila Mwananchi nchini kuwa na haki za kuendesha shughuli mbalimbali katika eneo lolote ndani ya Nchi lakini anatakiwa kuzingatia taratibu za kisheria.

View: https://youtu.be/dj1YEkzAZzs?si=0Bw9bcM2F_W_UcUV

"𝚆𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚎𝚗𝚐𝚒 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚜𝚕𝚒𝚖𝚒𝚊 𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚘𝚕𝚒𝚖𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚑𝚊𝚢𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚜𝚒𝚕𝚒𝚖𝚒𝚊 𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚝𝚘𝚔𝚊 𝚗𝚓𝚎 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚗𝚊 𝚜𝚒𝚘 𝚍𝚑𝚊𝚖𝚋𝚒 𝚠𝚊𝚕𝚊 𝚔𝚘𝚜𝚊 𝚖𝚝𝚞 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘 𝚗𝚍𝚊𝚗𝚒 𝚢𝚊 𝚖𝚒𝚙𝚊𝚔𝚊 𝚢𝚊 𝙽𝚌𝚑𝚒 𝚢𝚎𝚝𝚞 𝚑𝚊𝚒𝚓𝚊𝚕𝚒𝚜𝚑𝚒 𝚊𝚖𝚎𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚠𝚊𝚙𝚒 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚓𝚊𝚖𝚋𝚘 𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊 𝚗𝚒 𝚔𝚞𝚏𝚞𝚊𝚝𝚊 𝚞𝚝𝚊𝚛𝚊𝚝𝚒𝚋𝚞. "

"𝙺𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚠𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚎𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚜𝚑𝚒𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚞𝚊𝚏𝚊 𝚞𝚝𝚊𝚛𝚊𝚝𝚒𝚋𝚞, 𝚞𝚗𝚊𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚜𝚎𝚑𝚎𝚖𝚞 𝚠𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊 𝚞𝚗𝚊𝚓𝚞𝚊 𝚑𝚊𝚙𝚊 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚔𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚖𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊 𝚋𝚠𝚊𝚗𝚊 𝚊𝚞 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚝𝚊𝚓𝚒𝚛𝚒 𝚖𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊 𝚜𝚊𝚗𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚑𝚊𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚗𝚊𝚖𝚗𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘."anasema DC Mwema

Kutokuheshimu Mpango wa Matumizi Bora ya Aridhi

Mkuu wa Wilaya huyo, anasema kwamba Wilaya ya Kiteto inao mpango wa matumizi bora ya aridhi ambao anadai endapo ungekuwa ukiheshimiwa na kuzingatiwa migogoro ingewezekana kuepukwa kwa kiwango kikubwa.

"𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚢𝚊 𝚔𝚒𝚝𝚎𝚝𝚘 𝚒𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚒𝚔𝚒𝚝𝚊𝚓𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚜𝚞𝚛𝚊 𝚢𝚊 𝚖𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘 𝚢𝚊 𝙰𝚛𝚒𝚍𝚑𝚒, 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚗𝚊𝚝𝚊𝚔𝚊 𝚗𝚒𝚜𝚎𝚖𝚎 𝚓𝚊𝚖𝚋𝚘 𝚑𝚒𝚕𝚒 𝚕𝚒𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚊𝚕𝚒𝚝𝚞𝚏𝚞𝚛𝚊𝚑𝚒𝚜𝚑𝚒, 𝚜𝚒𝚘 𝚜𝚒𝚏𝚊 𝚗𝚣𝚞𝚛𝚒 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚒𝚗𝚊 m𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘, 𝚝𝚞𝚗𝚊𝚜𝚎𝚖𝚊 𝚜𝚒𝚘 𝚜𝚒𝚏𝚊 𝚗𝚣𝚞𝚛𝚒 𝚗𝚊 𝚝𝚞𝚕𝚒𝚔𝚞𝚓𝚊 𝚗𝚊 𝚔𝚊𝚞𝚕𝚒 𝚖𝚋𝚒𝚞 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 “𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚢𝚊 𝙺𝚒𝚝𝚎𝚝𝚘 m𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘 𝚑𝚊𝚒𝚗𝚊 𝚗𝚊𝚏a𝚜𝚒 m𝚊𝚎𝚗𝚍𝚎𝚕𝚎𝚘 𝚗𝚍𝚒𝚢o k𝚒𝚙𝚊𝚞𝚖𝚋𝚎𝚕𝚎”

Soma Wakulima 2000 Kiteto wamuomba Rais Samia aingilie mgogoro wa Ardhi (Hifadhi ya Makame)

Anaeleza zaidi "Tu𝚗𝚊𝚠𝚎𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚓𝚒𝚞𝚕𝚒𝚣𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚗𝚒𝚗𝚒 𝚖𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘 𝚒𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚒𝚔𝚒𝚎𝚗𝚍𝚎𝚕𝚎𝚊? 𝙺𝚒𝚝𝚎𝚝𝚘 𝚗𝚒 𝚖𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚗𝚒 𝚖𝚠𝚊 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚣𝚒𝚕𝚒𝚣𝚘𝚓𝚒𝚠𝚎𝚔𝚎𝚊 𝚖𝚙𝚊𝚗𝚐𝚘 𝚠𝚊 𝚖𝚊𝚝𝚞𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚖𝚊𝚣𝚞𝚛𝚒 𝚢𝚊 𝚊𝚛𝚍𝚑𝚒, 𝚝𝚞𝚗𝚊𝚢𝚘 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚖𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘 𝚗𝚊 𝚝𝚞𝚗𝚊𝚢𝚘 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚖𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚞𝚏𝚞𝚐𝚊𝚓𝚒 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚙𝚒𝚊 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣 𝚖𝚊𝚔𝚊𝚣𝚒, 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚖𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚑𝚒𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒"

𝙼𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘 𝚒𝚗𝚊𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚙𝚊𝚕𝚎 𝚋𝚊𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝚆𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚙𝚘𝚜𝚑𝚒𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚑𝚎𝚜𝚑𝚒𝚖𝚞 𝚖𝚒𝚙𝚊𝚗𝚐𝚘 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚢𝚊 𝚖𝚊𝚝𝚞𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚢𝚊 𝚊𝚛𝚍𝚑𝚒 𝚖𝚝𝚑𝚊𝚕𝚊𝚗𝚒 𝚔𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚎𝚕𝚎𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚖𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚖𝚊l𝚒𝚜𝚑𝚘, 𝙼𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊𝚜𝚑𝚒𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚑𝚎𝚜𝚑𝚒𝚖𝚞 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚑𝚒𝚕𝚘 𝚊𝚗𝚊𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘 𝚗𝚊 𝚝𝚊𝚢𝚊𝚛𝚒 𝚑𝚊𝚙𝚘 𝚞𝚗𝚊𝚣𝚊𝚕𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚖𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘"amesema DC Mwema
IMG_1073.jpeg

Anaongeza kuwa "𝙺𝚞𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚢𝚊𝚖𝚎𝚝𝚎𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚑𝚒𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒 𝙼𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚞𝚐𝚑𝚞𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘 au ufugaji 𝚑𝚊𝚙𝚘 𝚞𝚝𝚊𝚣𝚊𝚕𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚖𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘"

K𝚠𝚊 𝚖𝚏𝚊𝚗𝚘 𝚞𝚔𝚒𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚗𝚢𝚊𝚗𝚍𝚊 𝚢𝚊 𝚖𝚊𝚛𝚒𝚜𝚑𝚘 𝚢𝚊 𝙰𝚕𝚘𝚕𝚎 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 K𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚔𝚒𝚗𝚊𝚒𝚝𝚠𝚊 𝙰𝚖𝚎𝚒, 𝚞𝚟𝚊𝚖𝚒𝚣𝚒 𝚞𝚖𝚎𝚏𝚊𝚗𝚢𝚒𝚔𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚝𝚊𝚔𝚛𝚒𝚋𝚊𝚗𝚒 𝚎𝚔𝚎𝚛𝚒 𝟻𝟶𝟶, 𝚆𝚊𝚝𝚞 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚟𝚊𝚖𝚒𝚊 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚏𝚢𝚎𝚔𝚊 𝚔𝚊𝚋𝚒𝚜𝚊 𝚖𝚒𝚝𝚒 𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚊𝚗𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚏𝚊𝚗𝚢𝚊 𝚔𝚒𝚕𝚒𝚖𝚘.

Kukosekana kwa Uwajibikaji kwa baadhi ya Viongozi Ngazi za Vijiji

Remidius Mwema anaendelea kueleza sababu nyingine ambayo imekuwa chanzo cha migogoro ni baadhi ya viongozi Serikali za Vijiji haswa wenyeviti wa Vijiji kuwa sehemu ya migogoro kwa kutoa maeneo kinyume na Sheria na taratibu huku wengine wakishindwa kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao.

"𝚓𝚊𝚖𝚋𝚘 𝚕𝚒𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚗𝚒 𝚞𝚝𝚘𝚕𝚎𝚠𝚊𝚓𝚒 𝚠𝚊 𝚗𝚢𝚊𝚛𝚊𝚔𝚊 𝚔𝚒𝚗𝚐𝚞𝚖𝚎 𝚗𝚊 𝚞𝚝𝚛𝚝𝚒𝚋𝚞. M𝚏𝚊𝚗𝚘 𝚞𝚗𝚊𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚞𝚗𝚊𝚔𝚞𝚝𝚊 𝚖𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊𝚖𝚒𝚕𝚒𝚔𝚒 𝚎𝚔𝚊𝚕𝚒 𝟷𝟶𝟶 𝚊𝚗𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚙𝚎𝚠𝚊 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝙺𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒, 𝚕𝚊k𝚒𝚗𝚒 𝚔𝚠𝚊 𝚂𝚑𝚎𝚛𝚒𝚊 𝚗𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚝𝚊𝚗𝚘 𝚢𝚊 𝙰𝚛𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝙼𝚠𝚊𝚔𝚊 𝟷𝟿𝟿𝟿 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝙺𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚑𝚊𝚒𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚖𝚕𝚊𝚔𝚊 𝚢𝚊 𝚔𝚞𝚝𝚘𝚊 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚢𝚊 𝚎𝚔𝚊𝚛𝚒 𝟻𝟶, 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚞𝚝𝚊𝚔𝚞𝚝𝚊 𝚖𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚙𝚊𝚝𝚊 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚔𝚠𝚊 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝙺𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚢𝚊 𝚎𝚔𝚊r𝚒 𝟻𝟶."anasema DC Mwema
IMG_1104.jpeg

Anaongeza "𝙻𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚠𝚊𝚙𝚘 𝚟𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚠𝚊 𝚅𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚠𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚘𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚘 𝚗𝚍𝚒𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊 𝚖𝚊𝚖𝚕𝚊𝚔𝚊 𝚢𝚊 𝚔𝚞𝚐𝚊𝚠𝚊 𝚊𝚛𝚍𝚑𝚒 𝚋𝚒𝚕𝚊 𝚔𝚞𝚜𝚑𝚒𝚛𝚒𝚔𝚒𝚜𝚑𝚊, 𝚞𝚗𝚊𝚔𝚞𝚝𝚊 M𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎𝚔𝚒𝚝𝚒 𝚊𝚗𝚊𝚘𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚏𝚎𝚍𝚑𝚊 𝚊𝚗𝚊𝚜𝚊𝚒𝚗𝚒 𝚗𝚊 𝚑𝚞𝚢𝚘 𝙼𝚝𝚞 𝚊𝚗𝚊𝚜𝚎𝚖𝚊 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚜𝚑𝚊𝚙𝚎𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝙼𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎𝚔𝚒𝚝𝚒 𝚔𝚒𝚝𝚞 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚌𝚑𝚘 𝚗𝚒 𝚔𝚘𝚜𝚊 𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊"

"𝚃𝚞𝚖𝚎𝚋𝚊𝚒𝚗𝚒 𝚋𝚊𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝚆𝚎𝚗𝚢𝚎𝚟𝚒𝚝𝚒 𝚠𝚊 𝚟𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚠𝚊𝚜𝚒𝚘 𝚠𝚊𝚊𝚖𝚒𝚗𝚒𝚏𝚞 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚝𝚘𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚝𝚞 𝚔𝚠𝚊 𝚜𝚞𝚛𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚠𝚎𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚑𝚘𝚗𝚐𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚔𝚞𝚓𝚊 𝚔𝚞𝚐𝚑𝚊𝚛𝚒𝚖𝚞 𝚔𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚗𝚊 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚕𝚎𝚝𝚊 𝚖𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘.'

Kukosekana kwa Uadilifu kwa Baadhi ya Wataalamu

Mkuu wa Wilaya anabainisha wazi changamoto ambayo wameibaini kama sababu ambayo imekuwa ikipelekea uwepo wa migogoro kwenye Wilaya ya Kiteto, kwamba baadhi ya wataalamu ambao kwa nyakati tofauti wamehudumu katika Wilaya hiyo ikiwemo wataalamu wa aridhi wamekuwa wakitoa vibali bila kuzingatia taratibu.

"𝚂𝚑𝚒𝚍𝚊 𝚗𝚢𝚒𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚒𝚖𝚎𝚓𝚒𝚝𝚘𝚔𝚎𝚣𝚊, 𝚖𝚗𝚊𝚙𝚘𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚆𝚒𝚕𝚊𝚢𝚊 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚑𝚒𝚒 𝚟𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚖𝚗𝚊𝚝𝚊𝚔𝚒𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚞𝚊𝚍𝚒𝚕𝚒𝚏𝚞 𝚖𝚔𝚞𝚋𝚠𝚊" amesema DC

Anadai "𝙲𝚑𝚊𝚗𝚐𝚊𝚖𝚘𝚝𝚘 𝚗𝚢𝚒𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚗𝚒 𝚜𝚒𝚜𝚒 𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎𝚠𝚎 𝚟𝚒𝚘𝚗𝚐𝚘𝚣𝚒 𝚠𝚎𝚝𝚞, 𝚠𝚊𝚝𝚊𝚊𝚕𝚊𝚖𝚞 𝚠𝚎𝚝𝚞 𝚖𝚊𝚝𝚑𝚊𝚕𝚊𝚗𝚒 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚕𝚒𝚗𝚒𝚝𝚊𝚠𝚊 𝙽𝚐𝚊𝚋𝚘𝚕𝚘 𝚔𝚞𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚖𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘, 𝚕𝚊𝚔𝚒𝚗𝚒 𝚝𝚞𝚖𝚎𝚋𝚊𝚒𝚗𝚒 𝚋𝚊𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚊𝚊𝚕𝚊𝚖𝚞 𝚠𝚊 𝚊𝚛𝚍𝚑𝚒 𝚔𝚞𝚜𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚑𝚊𝚝𝚒 𝚣𝚊 𝚞𝚖𝚒𝚕𝚒𝚔𝚒 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚢𝚘 𝚠𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚓𝚞𝚊 𝚔𝚊𝚋𝚒𝚜𝚊 𝚗𝚒 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚢𝚊 𝚑𝚒𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚔𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚜𝚎𝚑𝚎𝚖𝚞 𝚢𝚊 𝚖𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘."

Anatoa mfano "𝚄𝚗𝚊𝚔𝚞𝚝𝚊 𝚖𝚠𝚊𝚗𝚊𝚗𝚌𝚑𝚒 𝚊𝚗𝚊𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚒𝚊 𝚗𝚒𝚗𝚊 𝚑𝚊𝚝𝚒 𝚑𝚒𝚒 𝚑𝚊𝚙𝚊 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚙𝚎𝚠𝚊 mtaalamu, 𝚗𝚒𝚗𝚊 𝚋𝚊𝚛𝚞𝚊 𝚢𝚊 𝚖𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎𝚔𝚒𝚝𝚒 𝚊𝚖𝚎𝚜𝚊𝚒𝚗𝚒 𝚗𝚊 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚕𝚒𝚖𝚊 𝚑𝚊𝚙𝚊,𝚜𝚊𝚜𝚊 𝚞𝚗𝚊𝚜𝚑𝚒𝚗𝚍𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚎𝚕𝚎𝚠𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚑𝚞𝚢𝚞 𝚖𝚝𝚊𝚊𝚕𝚊𝚖𝚞 𝚊𝚕𝚒𝚢𝚎𝚜𝚊𝚒𝚗𝚒 𝚊𝚔𝚊𝚖𝚔𝚊𝚋𝚒𝚍𝚑𝚒 𝚑𝚞𝚢𝚞 𝚖𝚝𝚞 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚠𝚊𝚔𝚊𝚝𝚒 𝚊𝚗𝚊𝚗𝚓𝚞𝚊 𝚗𝚒 𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚕𝚊 𝚑𝚒𝚏𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚑𝚞𝚢𝚘 𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚊𝚗𝚊𝚏𝚒𝚔𝚒𝚛𝚒𝚊 𝚗𝚒𝚗𝚒, 𝚔𝚠𝚊𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚔𝚞𝚗𝚊 𝚋𝚊𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚊𝚊𝚕𝚊𝚖𝚞 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚊𝚌𝚑𝚎 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚝𝚞𝚏𝚒𝚔𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚖𝚒𝚐𝚘𝚐𝚘𝚛𝚘.''

Ni hatua zipi wanazichukua kukabiliana na changamoto ya uwepo wa migogoro

Anaeleza kwamba mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, amekuwa akitumia muda mwingi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa na changamoto ili kubaini hali halisi kisha kuchukua hatua stahiki bila kuvunja Sheria na taratibu.
IMG_1086.jpeg

Mfano, anabainisha kwamba mara baada ya kubaini baadhi ya viongozi wa Serikali za Vijiji kuwa miongoni mwa wahusika wanaochangia uwepo wa migogoro, amedai kuwa wamekuwa wakiwapatia uelewa na kuwasisitiza uzingatiaji wa Sheria na taratibu.

"Kwa 𝚖𝚏𝚊𝚗𝚘 𝚝𝚞𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚞𝚌𝚑𝚊𝚐𝚞𝚣𝚒 𝚠𝚊 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚖𝚒𝚝𝚊𝚊 𝚖𝚠𝚊𝚔𝚊 𝚓𝚊𝚗𝚊 𝚝𝚞𝚖𝚎𝚠𝚊𝚙𝚊𝚝𝚊 𝚆𝚎𝚗𝚢𝚎𝚟𝚒𝚝𝚒 𝚠𝚊 𝚟𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚝𝚞𝚖𝚎𝚊𝚗𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚝𝚘𝚊 𝚎𝚕𝚒𝚖u 𝚔𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚎n𝚍𝚊𝚓𝚒 𝚠𝚊 𝚟𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒, 𝚂𝚎𝚛𝚒𝚔𝚊𝚕𝚒 𝚣𝚊 𝚟𝚒𝚓𝚒𝚓𝚒 𝚒𝚕𝚒 𝚔𝚞𝚓𝚞𝚊 𝚖𝚒𝚜𝚒𝚗𝚐𝚒 𝚢𝚊 𝚞𝚝𝚘𝚊𝚓𝚒 𝚠𝚊 𝚊𝚛𝚒𝚍𝚑𝚒" anasema DC Mwema

Aidha amesema kwamba kuhusu wataalamu ambao wanadaiwa kuwa sehemu ya kusababisha migogoro, anadai kwamba wameanza kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwasilisha majina ya wanao washtumu kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"𝙱𝚊𝚊𝚍𝚑𝚒 𝚢𝚊 𝚠𝚊𝚝𝚊𝚊𝚕𝚊𝚖𝚞 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚊𝚌𝚑𝚎 𝚝𝚊𝚢𝚊𝚛𝚒 𝚝𝚞𝚖𝚎𝚎𝚕𝚎𝚔𝚎𝚣𝚊 𝚟𝚢𝚘𝚖𝚋𝚘 𝚟𝚢𝚊 𝚜𝚑𝚎𝚛𝚒𝚊 𝚔𝚠𝚊𝚖𝚋𝚊 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚞𝚔𝚞𝚕𝚒𝚠𝚎 𝚑𝚊𝚝𝚞𝚊, 𝚗𝚒𝚖𝚎𝚔𝚊𝚋𝚒𝚍𝚑𝚒 𝚔𝚠𝚊 𝚃𝙰𝙺𝚄𝙺𝚄𝚁𝚄 𝚠𝚊𝚌𝚑𝚞𝚔𝚞𝚕𝚒𝚠𝚎 𝚑𝚊𝚝𝚞𝚊”anaeleza

'Waliojipatia ardhi kinyume wairejeshe'

Katika hatua nyingine amesema kwamba wameelekeza wale wote ambao walijipatia aridhi kinyume na utaratibu kuzirejesha kwenye mamlaka husika ili kuepuka mkono wa Sheria, ambapo anasisitiza kuwa atalisimamia kidete suala hilo.

"𝚃𝚞𝚖𝚎𝚎𝚕𝚎𝚔𝚎𝚣𝚊 𝚠𝚘𝚝𝚎 𝚊𝚖𝚋𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚕𝚒𝚓𝚒𝚙𝚊𝚝𝚒𝚊 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚔𝚒𝚗𝚢𝚞𝚖𝚎 𝚗𝚊 𝚞𝚝𝚊𝚛𝚊𝚝𝚒𝚋𝚞 𝚕𝚊𝚣𝚒𝚖𝚊 𝚠𝚊𝚘𝚗𝚍𝚘𝚔𝚎 𝚔𝚠𝚊 kuwa 𝚠𝚊𝚕𝚒𝚒𝚗𝚐𝚒𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚑𝚊𝚢𝚘 𝚖𝚊𝚎𝚗𝚎𝚘 𝚔𝚒𝚗𝚢𝚞𝚖𝚎 𝚗𝚊 𝚞𝚝𝚊𝚛𝚊𝚝𝚒𝚋𝚞 𝚗𝚊 𝚠𝚊𝚖𝚎𝚗𝚞𝚏𝚊𝚒𝚔𝚊 𝚔𝚠𝚊 𝚖𝚞𝚍𝚊 𝚖𝚛𝚎𝚏𝚞, 𝚔𝚠𝚊𝚑i𝚢𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚙𝚊𝚜𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚘𝚗𝚍𝚘𝚔𝚊 𝚗𝚊 𝚗𝚒𝚝𝚊𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚖𝚜𝚝𝚊𝚛𝚒 𝚠𝚊 𝚖𝚋𝚎𝚕𝚎 𝚔𝚞𝚕𝚒𝚜𝚒𝚖𝚊𝚖𝚒𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚕𝚒 𝚔𝚠𝚎𝚕𝚒"ameeleza

Soma Rais Samia atatembelea lini Jimbo la Simanjiro na Kiteto Mkoani Manyara! Kwani hajawahi kufika huko

Ukitaka eneo Kiteto zingatia taratibu kuepuka mkono wa sheria

Aidha ameedelea kutoa wito kwa wanaohitaji maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali kwenye Wilaya ya Kiteto kuwa makini ikiwemo kuzingatia taratibu zote za kisheria katika kupata ardhi na kwamba inapotokea changamoto ofisi zake zipo wazi kwa ajili ya kutoa usaidizi wa kisheria ili kuendelea kulinda mpango wa matumizi bora ya aridhi.

Kumbukumbu

Itakumbukwa Wilaya ya Kiteto kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ina ukubwa wa Kilometa za mraba 16,685 ikiwa na jumla ya wakazi laki 352,305, Tarafa saba Kata 23, Vijiji 63 na Vitongoji 278.

Wilaya hiyo kwa nyakati tofauti kumekuwa kukiibuka migogoro ya aridhi ikiwemo Wakulima na Wafugaji hali ambayo imekuwa ikipelekea athari mbalimbali ikiwemo uvunjifu wa haki za binadamu, kutokana na uwepo wa migogoro hiyo ili kuleta suluhu mnamo mwaka 2015 iliundwa Tume ya Waziri Mkuu ambayo ilishughulika na upimaji wa Vijiji jambo ambalo lilitajwa kupunguza kwa kiwango kikubwa migogoro ambayo ilikuwa inaleta athari zaidi.

Soma DOKEZO - √ - Wakulima 27 Wilayani Kiteto washikiliwa na Polisi kutokana na mgogoro wa Ardhi
 
Back
Top Bottom