Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Olivanus Thomas amegawa mbegu Bora na za kisasa za mihogo zijulikanazo kaa jina la Chereko, Mkuranga 1 pamoja na Tarikass 2 ili kuleta tija katika uzalishaji zao hilo la wilayani humo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa mbegu hizo mkuu wa wilaya huyo amesema wilaya ya Ludewa hasa upande wa tarafa ya Masasi una ardhi Bora kwa kilimo cha mihogo ila mbegu wanazotumia ni za asili na hazina ubora hivyo kwa mbegu hii itaenda kuongeza uzalishaji ambapo kwa Ekari moja ya shamba itazalisha kiasi cha Tani 9 mpaka 13 ukilingani na mbegu wanazotumia sasa ambazo wanavuna Tani 3 mpaka 5 kwa Ekari moja.
"Niliona kuna haja ya kuleta mbegu hizi kutoka kituo cha Tafiti za kilimo Tari Naliendele mkoani Mtwara ili kukuza uzalishaji wa zao hili ambapo mbegu hii inakabiliana na magonjwa mbalimbali yanayoikumba mihogo hivyo kupitia mbegu hizi nilizozigawa kwa kata tano za Tarafa ya masasi zitasaidia kuzalisha mbegu nyingine zaidi na kuendeleza kuzisambaza kwa wakulima wengine"