ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Huo ndio Ushauri wa DC Kwa Vijana wa Tanzania kwamba waache kulalamikia ugumu wa Maisha na kukosa Ajira badala yake wakalime maana huko ndiko Kuna utajiri.
My Take
Huyu Kwa nini asiache u DC aende kulima Ili awe Tajiri?
Bila kuwa Chawa hatoboi mtu
----
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Ng’waniduhu Malenya amewataka Wananchi hususani Vijana kutokaa vijiweni wakilalamika kuwa hakuna ajira na maisha magumu na badala yake wajiongeze kwa kujishughulisha na kilimo ambacho amesema kinalipa na wapo waliotajirika kupitia kilimo huku akisema Wilaya hiyo imepanga kufanya mapinduzi ya kilimo.
DC Ngollo amesema ili kuwafanya Wananchi washawishike kulima amenunua na kugawa bure majembe 500 kwa Wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua Sekta ya Kilimo nchini.
"Tunataka tufanye mapinduzi ya kilimo, Mh.Rais August 08,2023 alitangaza Mkoa wa Ruvuma kuwa tunaongoza kwa uzalishaji kwahiyo Mkoa wa Ruvuma ni Baba lao kwa uzalishaji wa chakula na Namtumbo tukiwemo”
Malenya ametoa majembe hayo wakati wa Kilele cha Jukwaa la Utambuzi wa Fursa za Kilimo, Biashara na Utalii (Namtumbo Kihenge) lililofanyika Namtumbo na kuhudhuria na Wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, pia Benki ya NMB ni miongoni mwa Wadau walioshiriki, Wadau wengine ni TFS, TIC, ASA, Nyerere National Park, n.k
Chanzo: Millard