Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Awali Mkandarasi aling’oa milango kwa madai ya kuwa hajalipwa gharama za kazi yake kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya amefafanua.
Kuhusu kilichotokea bofya hapa ~ Mkandarasi ang'oa milango ya kituo cha afya cha Bulige akilalamika kutolipwa pesa zake
MKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema suala hilo lilishamalizwa muda kidogo, kulitokea kutoelewana kati ya Mkandarasi na Mkurugenzi na hata wakati anang’oa milango kulikuwa na mazungumzo yanaendelea baina ya pande mbili.
Anasema “Mambo yaliwekwa sawa na mchakato wa malipo ukaendelea, milango ikarejeshwa na kila kitu kipo sawa.
“Sijui aliwaza nini huyo Mkandarasi, kwani walikuwa wameshakubaliana juu ya malipo, inawezekana alighafilika au labda kuna maneno alisikia, maana alikuwa anadai Ofisi ya Mkurugenzi, yeye anaenda kuondoa milango ambayo inatumiwa na watu wengi.
“Halikuwa jambo jema, tunachofurahia ni kuwa kila kitu kimekaa sawa na huduma zinaendelea kama kawaida.”