Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Amezitaka Taasisi Dini Wilayani Meatu kuwa Mfano wa kuigwa katika ujenzi wa vyoo Bora ili kuhamasisha Jamii kujenga vyoo Bora hatua itakayosaidia Wananchi kujihadhari na ugonjwa Hatari wa kipindupindu.
Ametoa maagizo na Rai hiyo alipofanya Ukaguzi wa usafi wa Mazingira katika Kaya na Taasisi mbalimbali ikiwemo Makanisa katika Kata ya Mbugayabanya katika kuadhimisha Siku ya Usafishaji Kimkoa Wilayani humo.
"Mtendaji nakuagiza shughuli za ibada katika makanisa haya zisimame mpaka watakapokuwa wamejenga vyoo Bora ili Wananchi wasipate magonjwa ya kipindupindu"
Watu 47 wameripotiwa kupata ugonjwa wa kipindupindu katika Kata ya Mbogayabanya huku 3 wakipoteza maisha tangu kuingia kwa ugonjwa huo katika Kata hiyo Wilayani Meatu.
Pia soma:
~ Katibu Tawala Simiyu: Elimu ya kujikinga na Kipindupindu kutolewa kwa Lugha ya Kisukuma na Kiswahili
~ Kipindupindu Simiyu kimeshamiri, kinaua ni hatari! Mbona Serikali haiweki wazi 'status' ipoje?
~ Wataalam wa Afya waingia mtaani kufanya jitihada za kudhibiti magonjwa ya kuhara Mkoani Simiyu