MLEMVYA RASHID
Member
- Aug 1, 2013
- 89
- 11
DC Mkwasa aelekeza walimu kujengewa mazingira mazuri
By Mwandishi wetu
19th february 2014
Mkuu wa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Betty Mkwasa
Madiwani na viongozi wa serikali za vijiji wilayani Bahi mkoani Dodoma
wametakiwa kuwawekea mazingira mazuri walimu wapya ili wasiondoke katika vituo vyao vya kazi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Betty Mkwasa, katika kikao
cha baraza la madiwani cha mapitio ya bajeti kwa mwaka wa fedha
2014/15 kilichofanyika wilayani humo.
Alisema kuwa endapo watafanya hivyo kutasaidia walimu wanaopangwa
katika wilaya hiyo wasiondoke kwa kisingizio kuwa mazingira sio rafiki
kwao.
Mkwasa alisema kuwa mwaka juzi alihimiza utaratibu huo na ulisaidia kwani walimu wengi waliopangiwa kufundisha wilayani humo
walifurahia mazingira.
Alisema kuwa hali hiyo imewasaidia walimu wengi kutoondoka katika vituo vyao vya kazi.
"Msimu wa ajira mpya za walimu nyie madiwani, watendaji na wenyeviti wa
serikali za vijiji, naomba tutumie utaratibu wetu tuliofanya mwaka
juzi, alisema Mkuu.
Alifafanua kuwa walimu hao walipokelewa na kutafutiwa nyumba nzuri za kuishi na hivyo wengi wao walibaki kwenye vituo vyao.
"Mwaka jana mimi sikufuatilia, na ninyi wenzangu hamkuendeleza
utaratibu wetu, matokeo yake walimu wengi waliopangiwa Bahi waliondoka," alisema.
Aliongeza kuwa ni vyema utaratibu huo uwe endelevu ili wilaya hiyo isiwe na
upungufu wa walimu kwa sababu ya kukimbia mazingira na kukosa nyumba
nzuri za kuishi.
:baby:Katika hatua nyingine Mkwasa amewataka watendaji kuhakikisha ujenzi wa
maabara za shule za sekondari wilayani humo unakamilika ifikapo mwezi
Juni mwaka huu.:smile-big: