DC Mpogoro, nilidhani ni habari njema kwa wenye maghorofa chakavu kariakoo kuyavunja, huyu kaamua kuvunja, wewe umemkasirikia na kumuweka ndani saa 48

DC Mpogoro, nilidhani ni habari njema kwa wenye maghorofa chakavu kariakoo kuyavunja, huyu kaamua kuvunja, wewe umemkasirikia na kumuweka ndani saa 48

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Hii habari inashangaza, mtu kaona ghorofa lake ni chakavu, lina nyufa, na linatumiwa na watu na juu ni stoo ta mizigo. Kaamua kulivunja pengine ajenge lililo imara zaidi.

Mkuu wa Wilaya wa eneo ambalo yalitokea maafa ya ghorofa kuanguka, anamkamata na kumuweka ndani. Ebooo! Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya alitaka likae hapo mpaka liue watanzania wengine?

Hajaona Samia na serikali nzima ilivyohangaika na kuacha shughuli zote kwa sababu ya maafa katika hiyo hiyo Wilaya yake? Hajaona familia zikilia kupoteza wapendwa wao? Hajaona mitaji ya watu ilivyokufa?

Halafu unamuweka ndani saa 48! Hivi mtu anayeokoa maisha ya wenzake ni wa kuwekwa ndani? Mtu anavunja jengo lake, na ana vibali vya Manispaa, unamuwekaje ndani? Mbona Mkurugenzi hajalalamika? Kama kuna kosa katika kibali si ushughulike na Mkurugenzi?

Hei, come on, Mr. DC, sense zako uliziacha Iringa au Njombe? au unatafuta hela za krismas? Nyambiti kabisa
Screenshot_20241222-070301.jpg
 
ninavyojua hao ma dc wanachaguliwaga watu wenye elimu sasa sitaki kuamini hizi ndizo akili za wasomi wetu..... labda kama kuna mgogoro na kama upo jengo limeonyesha udhaifu ni kusitisha matumizi mgogoro uishe kila mtu afanye yake kuwekana ndani mbona ni mbinu za kizamani sana...... japo tz tupo miaka 200 nyuma ya dunia
 
Hilo jengo kama una d mbili kutoka pale kwa kobazi mkuu mjini Tehran utaona wazi kuna mgongano wa kifamilia , lakini hata iweje lile jengo kweli ni bovu halifai kabisa hata kama wanataka kukomoana ila upande unaosimamia kubomoa uko sahihi
 
Nilitegemea wahariri wa balance habari toka pande zote mbili (Dc aseme pia kwanini kazuia) kabla ya kuipandisha hewani. Sambamba na hayo bado sio sahihi kuzuia jengo kuondolewa kama sio salama kwa watumiaji pamoja na jamii inayozunguka eneo hilo.
 
Hilo jengo kama una d mbili kutoka pale kwa kobazi mkuu mjini Tehran utaona wazi kuna mgongano wa kifamilia , lakini hata iweje lile jengo kweli ni bovu halifai kabisa hata kama wanataka kukomoana ila upande unaosimamia kubomoa uko sahihi
Ndio
 
Back
Top Bottom