DC Muro: Wadau kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti Ikungi

DC Muro: Wadau kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti Ikungi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
WADAU KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI IKUNGI

Serikali ya wilaya ya Ikungi imefanikiwa kuwaunganisha wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya Maendeleo ya kilimo

Hatua hiyo imekuja baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha majadiliano ya mwisho ya namna ya kuwawezesha wadau waliochukua mashamba yenye ukubwa wa hekari 4,500 kwa ajili ya Kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti

Tayari serikali imewezesha kuundwa kwa kikosi kazi (task force)inayojumuisha wadau wanaolima alizeti, serikali, Halmashauri kupitia afisa kilimo na afisa ardhi, pamoja na taasisi zote za kifedha zikiwemo benki za bishara kwa ajili ya kutatua changamoto zilizojitokeza

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi
01/11/2021

IMG-20211101-WA0225.jpg
 
Back
Top Bottom