Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva amefika na kuripoti rasmi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack leo tarehe 05 Septemba, 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva ameripoti katika kituo chake cha kazi cha Wilaya ya Lindi baada ya kile cha awali Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe ikiwa ni baada ya mabadiliko ya kawaida aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 02 Septemba, 2024.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack amemkaribisha DC Mwanziva katika Mkoa Lindi ili kuendeleza jukumu la kumsaidia kazi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Kuwatumikia wananchi wa Lindi.
#KaziIendelee