Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ambaye pia ni Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewasihi wanachama wa CCM waliokosa uteuzi kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi wa Novemba 27, 2024, kuacha 'makandokando' na fitina badala yake waungane pamoja kuwatetea na kuwaombea kura wanachama wa CCM walioteuliwa na kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa.
Magoti ameyasema hayo akizungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kisarawe, kilichoketi kufanya tathmini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo baadaye Novemba 27, 2024.
Magoti ameyasema hayo akizungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kisarawe, kilichoketi kufanya tathmini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo baadaye Novemba 27, 2024.