DC Rorya apiga marufuku uchomaji mkaa

DC Rorya apiga marufuku uchomaji mkaa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MKUU wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga amepiga marufuku uchomaji mkaa wilayani humo na kuonya serikali itawachukulia hatua kali baadhi ya wazazi wanaotumikisha watoto wadogo katika shughuli hizo.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati wilaya hiyo ikianzisha mkakati maalum wa utunzaji mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na upandaji miti.

Alisema katika siku za karibuni kuna taarifa kutoka maeneo ya vijijini wilayani humo kuhusu vitendo vya baadhi ya wazazi wasio waaminifu kuwatumikisha watoto ambao wanasoma shule mbalimbali katika shughuli za kibiashara ikiwamo uchomaji mkaa.

Aliwaagiza makatibu tarafa na kata pamoja na viongozi wa vijiji kuwasaka wazazi wote wanaotumikisha watoto kuchoma mkaa wakati wa likizo ya mwisho wa mwaka ili wachukuliwe hatua za kisheria.

"Kwa sasa wilayani Rorya hakuna miti, serikali inafanya uhamasishaji kwa wananchi juu ya matumizi ya nishati mbadala na kuepuka vitendo vya kukata miti ovyo hali inayoweza kusababisha mabadiliko ya tabianchi," alisema.

Odunga aliwaagiza maofisa kilimo wote wa kata kuwaelekeza wananchi katika maeneo yao kufanya kilimo bora cha mazao ya chakula na biashara yaliyo rafiki kwa mazingira na kuepuka kukata miti ya asili ovyo.

Aliwataka wananchi wanaofanya biashara ya mazao ya misitu kupata kibali kutoka ofisi za misitu na kuepuka kusafirisha mazao hayo kwa njia zisizofaa.

"Tunawashauri wananchi wote wilayani hapa wenye nia ya kufanyabiashara za mazao ya misitu wafuate utaratibu halali uliowekwa kisheria ikiwamo kupata kibali kutoka ofisi ya misitu na kuepuka uharibifu wa mazingira," alisema.
 
Serikali ingerahisisha upatikanaji wa vyanzo bora vya nishati na mbadala wa mkaa kabla ya kukurupuka kuzuia mkaa.
 
Duh, hata tufanyeje hatuwezi kuzuia matumizi ya Mkaa kwa nchi ambayo ni third country Kama Tanzania
 
Sasa wale vyakula vibichi, gesi bei juu, umeme ni balaa.Muwe nafikiri kabla ya kusema nyie wateule.
 
Serikali wanatakiwa kuacha biti, wawape tu nishati mbadala itakayokuwa nafuu kwaajiri ya matumizi yao. Hawa wananchi wanachokosa ni elimu, na msaada kutokana na hali zao za kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali wanatakiwa kuacha biti, wawape tu nishati mbadala itakayokuwa nafuu kwaajiri ya matumizi yao. Hawa wananchi wanachokosa ni elimu, na msaada kutokana na hali zao za kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DC ukitumbuliwa na JPM utamlalamikia nani? Maguful ni mtetezi wa wanyonge wewe unapingana na wenyonge! Hakuna tajiri anae hangaika na mikaa,mkaa in Dalili mojawapo ya umasikini, hivyo basi mkuu wa wilaya buni njia ya kuuondoa umasikini na sio matokeo ya umasikini.
 
Back
Top Bottom