#COVID19 DC Sabaya: Msiogope kusalimiana kwa mikono kisa hofu ya Corona. Corona ni biashara ya watu wachache inayopaswa kutizamwa kwa macho matatu!

#COVID19 DC Sabaya: Msiogope kusalimiana kwa mikono kisa hofu ya Corona. Corona ni biashara ya watu wachache inayopaswa kutizamwa kwa macho matatu!

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Mkuu wa wilaya ya Hai,Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya amewatoa hofu wananchi wa wilaya hiyo kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kuwataka wasiogope kusalimiana kwa mikono kama ilivyo desturi ya kiafrika kwa kuwa hofu ndio inayokatisha maisha yao.

Sabaya ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la huduma za kinywa na meno wakati akiongea na wafanyakazi wa halmashauri ya Hai ,ambapo alisema ugonjwa wa Corona ni biashara ya watu wachache inayopaswa kutizamwa kwa macho matatu.

Alisema kumekuwepo dhana yenye mtazamo tofauti juu ya Kila anayefariki dunia kuelezwa kuwa amekufa kwa Korona Jambo hilo linasababisha wananchi kujawa na hofu na wengi wao kupoteza maisha nakusisitiza kuwa wilaya hiyo ipo salama.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kujifukiza majani yaliyofukizwa na mungu na kufanywa dawa ya kuwaponya na kuepuka matumizi ya chanjo ambayo ni biashara ya Mabeberu na si salama sana.

Kwa upande wake naibu waziri wa TAMISEMI,David Silinde aliwataka wananchi kuondoa hofu kwa taarifa za uongo dhidi ya ugonjwa wa Corona Ila wachukue tahadhali za msingi zitakazowaimarisha .

Aliitaka jamii kuzingatia maelekezo ya serikali hasa yanayotolewa na Rais John Magufuli kuwa ugonjwa wa Corona unatibika kwa nguvu za mwenyezi mungu .

Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya hiyo ,Dkt Irene Haule alisema Jengo hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 82 fedha ambazo Imetokana na mapato ya ndani.

Hata hivyo alisema kumekuwepo.na changamoto ya upungufu kwa watumishi wa Afya wilayani humo hasa katika kitengo Cha huduma ya kinywa na meno kwani Kati ya watumishi 10 wanaohitajika kwa Sasa Kuna watumishi watatu tu Jambo ambalo linaleta changamoto kubwa katika utoaji huduma ya kinywa na meno.

IMG-20210211-WA0132.jpg
IMG-20210211-WA0133.jpg
 
Itakapokuja Covid ingine ndo ataaanza kulia nayo kikweli kweli maana naona bado anacheka nayo
 
Ole Sabaya hivi kukiwa hamna Korona na ukawaambia watu wasisalimiane kwa mikono na kuchukua tahadhari unapata hasara gani, Angalau kwa kipindi hiki kipite?

Ni bora uwaambie watu wachukue tahadhari hata kama hamna korona (kwa mawazo yako lakini) kuliko kuwaambia watu wasichukue tahadhari alafu bahati mbaya Korona ikawepo.

Viongozi tujipe nafasi kama viongozi wenye uwezo wa kulinda uhai wa watu.
 
Ole Sabaya hivi kukiwa hamna Korona na ukawaambia watu wasisalimiane kwa mikono na kuchukua tahadhari unapata hasara gani, Angalau kwa kipindi hiki kipite? Ni bora uwaambie watu wachukue tahadhari hata kama hamna korona (kwa mawazo yako lakini) kuliko kuwaambia watu wasichukue tahadhari alafu bahati mbaya Korona ikawepo. Viongozi tujipe nafasi kama viongozi wenye uwezo wa kulinda uhai wa watu.
Hawa ndo viongozi wetu. Kwani watu wasiposalimiana kwa mkono watakosa nini ?
 
Yaaani ni bora ukaacha tu kuongelea hizi habari kwa uongo...aongee siasa tu aache kuwakera watu, sijui anajua kuna familia ngapi saa hzi wana misiba ya waliokufa kwa changamoto ya upumuaji...DAB liiletea zereu..ikamtenda [emoji23][emoji23]
Hawa watu wamelaaniwa sn
 
Kama taifa tumekwama tunaongozwa na watu waajabu Sana..
Majuto badae
 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya amewatoa hofu wananchi wa wilaya hiyo kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kuwataka wasiogope kusalimiana kwa mikono kama ilivyo desturi ya kiafrika kwa kuwa hofu ndio inayokatisha maisha yao...
Huko Hai vifo vya corona ni kila kona ya wilaya.
 
Back
Top Bottom