DC Temeke amekifungia chuo cha Kewovac kinachotoa elimu ya uuguzi na ukunga Mbagala kutokana na ubovu wa mazingira ya chuo

DC Temeke amekifungia chuo cha Kewovac kinachotoa elimu ya uuguzi na ukunga Mbagala kutokana na ubovu wa mazingira ya chuo

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amekifungia chuo cha Kewovac kinachojihusisha na utoaji wa elimu ya uuguzi na ukunga kilichopo Mbagala Charambe kwa kutokidhi vigezo vya utoaji wa elimu hiyo na ubovu wa mazingira ya chuo hicho.

DC Mapunda ameagiza kukamatwa mara moja kwa mkurugenzi wa chuo hicho na wasaidizi wake ili kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwemo kukiuka agizo la Serikali kukifungia chuo hicho hadi pale kitakapoweka mazingira rafiki kwa ajili ya wanafunzi kusomea.

Soma pia: Dkt. Pius Chaya ameomba Serikali kupeleka chuo cha uuguzi na ukunga kwa ngazi ya astashahada

"Ofisi inayosimamia uendeshaji wa vyuo hivi, ukichunguze chuo hiki vizuri, ninafunga rasmi kituo hichi leo hii kuanzia sasa hakitatoa huduma" alisema Dc Mapunda

Makosa mengine yanayomkabili mkurugenzi huyo ni pamoja na kutofuata mtaala wa Serikali unaoagiza elimu ya uuguzi na ukunga kufundishwa kwa miaka miwili na si mwaka mmoja kama kinavyofanya chuo hicho.​
Screenshot 2024-11-22 120113.png

Screenshot 2024-11-22 120048.png


Chanzo: Clouds Media
 
Vipo vyuo ving vya kisng vya namna hiyo, vingine havijasajiliwa kbs, vingine miundombinu mibovu, wasimamizi wa vyuo wamo maofisini tu
 
Back
Top Bottom