mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amekwepa kujibu swali kuhusu nani aliyehusika katika madai ya utekaji wa Edgar Mwakabela, maarufu Sativa.
Bomboka alikwepa swali hilo akiwa katika kipindi cha Medani za siasa cha runinga ya Star TV, huku akieleza kuwa wajibu wa Serikali ni kulinda raia na mali zao.
Msingi wa Bomboko kuulizwa swali hilo ni kwa sababu Sativa aliyedaiwa kupotea Dar es Salaam Juni 23, 2024 na kupatikana Alhamisi Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na majeraha mwili ni mkazi wa Wilaya ya Ubungo.
“Jambo hili sasa hivi halipaswi kujadilika katika kipindi hiki,”amesema DC Bomboko, mtangazaji alipoendelea kumuuliza kuhusu muhusika wa kitendo hicho alisisitiza, “no coment (sina la kusema).”
Hata hivyo akizungumzia tukio la kupatikana Sativa mkoani Katavi, Juni, 2024, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kaster Ngonyanyi alisema jeshi hilo linafanya uchunguzi kuwabaini waliohusika.
Pia soma
- Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’
- Kamanda wa Polisi Katavi: Edgar Mwakabela (Sativa255) anasema alichukuliwa Dar hadi Arusha na kisha kutupwa Katavi
- Alichosimulia Edgar Mwakabela "Sativa" kuhusu waliomteka na kumpiga Risasi ya Kichwa