DC Zainabu: Nawapa heshima wanawake wote ambao wanajishughulisha na wanajua uchungu wa kutafuta pesa, nawapenda

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amefunguka na kudai anawaheshimu wanawake wenzake wanaojishughulisha kutafuta pesa kwa namna moja ama nyingine huku akiwataka wasiwape upenyo baadhi ya watu ambao wanataka kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Bi. Zainab ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo baada ya kuwepo kwa imani potovu kwa baadhi ya wanaume ambao wanawakatazia wanawake zao kutojihusisha na ufanyaji kazi wa aina yeyote ile.

"Heshima ya mwanamke ni kujishughulisha na kuingiza kipato chako mwenyewe, haijalishi umeajiriwa au kujiajiri. Haijalishi unauza Mama Ntilie, unajishughulisha na kilimo au biashara yoyote ile. Kikubwa heshimu unacho kifanya na usimpe nafasi mtu kudharau kinacho kuingizia rizki. Nawapa heshima wanawake wote ambao wanajishughulisha na wanajua uchungu wa kutafuta pesa, nawapenda", amesema Mkuu wa Wilaya Zainab.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amesema hayo ikiwa kama ni ishara ya kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huwa inaadhimishwa kila ifikapo Marchi 8 ya kila mwaka na kudai ataendelea kufanya hivyo mpaka kufika tarehe hiyo.

Credit: EATV
 
mange je?
 
Huyu DC anajielewa mpaka alimpa ruhusa mume.wake kuongeza mke ili wasaidiane majukumu maana mume anafanya kazi dar yeye yupo pangani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…