DCs wapanguliwa na kustaafishwa

Huyu jamaa kutoka TRA,Chali Ubunge(CCM-Tarime) mpaka Ukuu wa Wilaya? Si Mwingine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza). Kweli Tanzania kila kitu kinawezekana ukizingatia pesa aliyopoteza pale Tarime kwenye mchakato wa uchaguzi Tarime, na alikuwa anakaribia kustaafu pale TRA, ngoja akapumzikie kwenye ukuu wa wilaya. Wasiwasi wangu isiwe ni sehemu ya kurudushia ile pesa yake aliyotupa kwa rushwa ili achaguliwe.
 
JK ni fisadi na ndiyo maana anaendelea kulea mafisadi. Francis Isaac alitimuliwa UVCCM kwa tuhuma za ufisadi, bado kambeba kama alivyo na kumpa Ukuu wa Wilaya, hivi kweli huyu Rais wetu yuko serious na vita ya mafisadi? Anapeleka msg gani kwa mafisadi wengine? Kwamba endelee kufanya ufisadi mkigundulika nitawahamishia sehemu nyingine! Kaazi kweli kweli.
 


Mimi masikitiko yangu ni kwmba form IV wamejazana humo, mfano ni Anatory choya, huyu alikuwa mbunge wa biharamulo magharibi 1995-2005. Aliwahi kufanya kazi uhamiaji sasa eti mkuu wa wilaya...jamani JK sijui anawashauri wa aina gani???
 

Kaaazi kwelikweli!!!!!!!!!!!!!! Hii ni dalili kuwa hata wale mafisadi waliojiuzulu watakuwa wanaandaliwa maeneo ya kujidai mahali pengine! Muungwana hana aibu!
 
Ni usanii na wizi mtupu!!! 🙂
 
Wakuu, swali langu ni kwamba "Mbona lawama zote anapewa JK, je ni yeye aliamua nani awe wapi au ni washauri wake?". Kama ni washauri wake (ambalo naamini ni sawa sababu Raisi hawezi chagua wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi, maPS, etc etc etc kutokea kichwani pake pekee) then tusimlaumu sana manake ni "shared responsibility" hiyo, washauri wanapendekeza yeye ana approve!!

Kurudi kwenye mada ni kwamba kwa vile siwafahamu wote, basi nijiunge kulaumu kwenye mapungufu (kama yapo)!
 
Hayo ni maandalizi ya 2010.Lazima aweke ccm makada.
Hivi ingekuwaje pale ambapo nafasi za u-DC zinatangazwa, watu waombe kama kazi nyingine. Nakumbuka enzi za nyumba Mkapa alikuwa ameanzisha utaratibu wa ma-DED kuomba kazi badala ya kuteuliwa ingawa Kikwete alikuja kuiondoa!
 
Nina swali wan JF, I thought miaka yote Waziri Mkuu nndie anayeteuwa maDC au nimekosea?
 
Kuna wazee ambao walishapoteza kina shelutete du yule ndio kimeo kabisa...pia yule wa bagamoyo..pia waliowekwaga na sumaye hasa wamama kibaoo walikuwa headteachers kuna kazi kubwa....
 
nimekumbuka maneno ya mkapa,watanzania wana wivu wa kike..kiutendaji frank isac hana tatizo kabisa na kutolewa kwake pale ilikuwa kwa makubaliano kama haya!
Any way,Mercy Silla amefanya nini?ukiangalia kabisa utaona ameandaliwa mtu..
Patrick sere anaweza kupewa nafasi ya Mercy ,
Hv hawa wanajeshi wastaafu na ukuu wa wilaya wapi na wapi?au CDF Naye ana nafasi zake
 
..nashangaa kanda2 na Chuma hawajaleta hoja zao za udini ktk teuzi hizi.
 
Huu je ni wivu wa kiume?
 
Yetu macho watu ni walewale na tabia zao zilezile,tofauti ni majina na sehemu.
 
Tunaomba full list ya waliohamishwa....maana jumla waliohamishwa wapo 54 taarifa haijakamilika
 
Huu je ni wivu wa kiume?

Ona sasa unaposhindwa kujenga hoja,hayo yametoka wapi?mie nimeuliza kwa nia njema ili nijue,au na wewe unataka uwe maarufu tu kupitia kupinga hoja za Gembe?

Babu yako Mwanakijiji huwa ana kumsemo flani ka ukweli sana,kila mtu anaweza kuandika maneno ila kupanga maneno ni sanaa wanaoiweza wachache !wewe siyo mmoja wao!
 
Ama kweli nyani haoni kundule!kama bodi twende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…