Kwa wilaya zilizopo mipakani nadhani kwa sababu za kuisalama na sometimes kuibabe,inabidi apewe mwanajeshi (hili nililishuhudia wilaya za Kigoma na kagera)
Mashimba hakustahili kustaafishwa bali kufukuzwa. Akiwa DC pale Kyela katika mengi alofanya ni pamoja na;
1. Kwa kushirikia na RC Mbeya wamefukarisha kina mama wauza mchele kwa kuzuia harambee yao huku wakiwa wametumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuiandaa, kisa mgeni rasmi Prof Mwandosya.
2. Kuwahadaa wafanyakazi wa Kiwira Coal Mine kwamba anashughulikia matatizo yao kumbe anatayarisha mazingira ya rushwa, alizawadiwa VX kwa laki sita
3. Kukosa adabu mbele ya Mkuu wa Kaya alipokuwa ziarani katika Mkoa wa Mbeya mwaka jana. Alifanya utani kwa kupokea simu wakati anamsomea Rais taarifa ya wilaya na kusema "Hujui kuwa niko na bosi wangu, Mweshimiwa watu wengine bwana!" Alirudia mara mbili kitendo hicho, bw mkubwa aliishia kucheka!
4. Alifumaniwa na mkewe akiwa na hawara nyumbani kwake (DC) habari zikazaaga mji wote wa Kyela kwani haikuwa siri na walifika hadi kituo cha p[olisi kusuluhisha.
Ni wazi kwa matukio hayo amevumiliwa sana. Hivi sasa katika Mji wa Kyela watu wanasheherekea.
Kwa kweli ma DC wa KJ wanazua maswali mengi
Ouwiii! Awe karibu zaidi na mkubwa. Maana kufungafunga safari za Korogwe kuna matatizo yake.
Mkuu Jasusi,
Inaelekea wewe na Mwawado kuna jambo mnajua zaidi lakini hamtaki kutuhabarisha.
Wakubwa wako wengi, ni nani huyo mkubwa wa Chimwano?
Unatutega?* si wewe unayejidai CCM damu sasa unamuuliza nani na nyie ndiyo mliandika katiba na hamtaki* katiba mpyaCCM ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!- Wakuu hivi kweli tunahitaji Wakuu wa wilaya Tanzania?FMES!
Dk. Rehema Nchimbi (Newala)
Wakuu huyu ni Nchimbi yupi?
Dr.Nchimbi?PhD nzima unakuwa mkuu wa wilaya,watoto wetu Chuo kikuu je?
..nashangaa kanda2 na Chuma hawajaleta hoja zao za udini ktk teuzi hizi.
Habari zilizopatika na ni kuwa DCs wamapanguliwa na wengine kustaafishwa bila shaka tuna wanachama wa JF waliopewa SHAVU.
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).
Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).
Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).
Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).
Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT
JokaKuu....Nilipoona post yako nikabaki kucheka tu...Tunahaja gani ya kuhoji wakati hakuna sababu hizo?...Mara nyingi wanaohoji ni wale ambao wanapoona tu teuzi zinapokwenda kwa waislam...!!!
Its Good watu wanahoji utendaji wa wahusika...
ES....kimsingi hatuna haja ya kuwa na wakuu wa Wilaya wala wakuu wa Mikoa...ni taratibu ambazo tumerithi kutoka kwa wakoloni...bahati mbaya pia hawa wakuu pamoja na kuteuliwa kwao kuwasaidia Rais na Wazir Mkuu, wamekuwa si wasaidizi makini zaid wamekuwa ma-opportnist fulani
Ipo Haja ya kureview mambo mengi ktk Cooperate Government studies. The same na utitiri aliousema Philimone Michael ktk mada fulani kuhusu znz...same na na Mainland tumejaza vyeo Lukuki sana. utendaji zero...
ktk Wakati huu wa Uchumi Legevu, wenzetu wa Kenya wameweka mkakati wa kutoajiri kwa nafasi ambazo hazina umuhim wa haraka...atleast tungeona GOT nayo inaanza na wakuu wa wilaya....i.e. Mfano DSM tuna wakuu wa wilaya 3 na Mkuu wa Mkoa 1,(total 4) tungeweza kabisa alau kuwa na wakuu wa wilaya 2, then mkuu wa Mkoa anakuwa pia mkuu wa wilaya ya Ilala....atleast tungepungza wakuu wengi sana...
Anaweza kuwa ni Medical Assistant, si nao wanajiita Dr.
ES....kimsingi hatuna haja ya kuwa na wakuu wa Wilaya wala wakuu wa Mikoa...ni taratibu ambazo tumerithi kutoka kwa wakoloni
Anaweza kuwa ni Medical Assistant, si nao wanajiita Dr.
Elizabeth Mkwasa kahamishiwa BAHI - Dodoma karibu na Ikulu ya Chamwino!!
Out of curiosity .... Chamwino ni Ikulu ndogo ya JK, kwa hiyo ndo kusema Elizabeth Mkwasa ni nanihiino ndogo ya Ikulu?
Mkuu Keil,
Umeniwahi, nilitaka kuuliza swali hilo hilo, anyway tuache tusije tukaambiwa tunadhalilisha dada zetu.
Ouwiii! Awe karibu zaidi na mkubwa. Maana kufungafunga safari za Korogwe kuna matatizo yake.
ok asante nilikuwa mbali kidogoIpole upo wapi wewe?????hii sio habari mpya atii...imetoka jana mchana...