Hatimaye Bangala atua mikono ndani ya Viunga vya Chamazi Complex, matajiri hawa wameamua kweli kweli. Tutarajie makubwa ligi ya Msimu huu na kimataifa.
Bangala atawasaidia Azam, ila kwasasa Yanga ilihitaji mchezaji mzuri zaidi yake.
Aliondoka Mukoko akiwa MVP,akaondoka Feisal na sasa ameondoka Bangala kama MVP lakini taabu iko palepale.
All the best Bangala!
Kuondoka kwake ni faida kubwa kwa mabeki wazawa Yanga wanaocheza pia Taifa Stars. Kuna muda Bangala alikamata mkoba kisawasawa ikawa Nondo Le Kapiteni hatihati kutua kwa mkopo Lipuli au Sahare Big Stars! Benchi lilipata joto lake la kutosha!
Yanga ni timu Kali kwa Sasa inacheza kitimu mpira wa Kasi wenye njaa ya ushindi hata Mimi nikienda na kitambi changu naziba pengo lake fasta tu kama tulivyomsahau Feisal!