Death surprise

Death surprise

Capt Nemo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
1,445
Reaction score
680
Jamaa mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kuonewa alikula mchongo na mzikaji wa gereza jinsi ya kumtorosha. Basi wakakubaliana kuwa siku jamaa akisikia kengele ya msiba pale gerezani basi akimbilie kwenye chumba cha maiti ambamo atakuta jeneza lipo tayari katikati ya chumba. Kwa kuwa majeneza yanakuwa ready-made na yametengenezwa kuweza kuaccomodate mwili wa ukubwa wowote basi mfungwa angeingia mle ndani

wakakubaliana kuwa baadae mzikaji angekuja na kupigilia misumali kufunga jeneza kabla ya jeneza kupelekwa makaburini ambapo dakika 20 baada ya kuzikwa mzikaji angekuja na kumfukua.

Basi siku ya siku mambo yakaenda kama ilivyopangwa jamaa akaingia kwenye jeneza, akasikia misumali inagongwa kulifunga na safari ya makaburini ikaanza. walipofika kama kawaida jeneza likafukiwa jamaa akabaki anasubiri dakika 20 mzikaji aje kumfukua. mara ikapita kama nusu saa mzikaji haokei na joto kule chini likaanza kusumbua jamaa..

mara wazo likamjia amuangalie ni mfungwa gani alikuwa amekufa siku hiyo..akajitahidi kukodoa macho gizani akamfunua marehemu kichwani.. kutahamaki akakutana na sura ya MZIKAJI!!!! aliyetakiwa kumfukua!!!!
 
Story nzuri japo ilishaletwa hapa tayari
Labda iwe maalum kwa wale ambao hawakubahatika kuisoma
 
Back
Top Bottom