Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
DEBORA TLUWAY AFIKA TUNGUU, CHUO CHA UVCCM
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa, Komredi Debora Joseph Tluway tarehe 15 Desemba 2024 ametembelea Chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM Tunguu Zanzibar na kuona miradi na mikakati mbalimbali inayotekelezwa ikiwemo Ufugaji wa Kuku wa Mayai na ujenzi wa majengo Chuoni hapo ambao unaendelea sasa hivi.
Debora Joseph Tluway ameweka jiwe la msingi la Ofisi ya Kundi la Umoja wa Vijana wa CCM K.K.V Kiomba - Mvua ambapo amechangia Matofali 500 na viongozi wengine pia Wabunge na Madiwani wamechangia K.K.V ili kusaidia ujenzi wa kisima cha maji
"Mwaka 2025 kuna uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Naomba tuwape nafasi wagombea wote wanaotokana na CCM. Muda ukiwadia twende Tukajiandikishe kwenye Daftari la Mpiga Kura ili tuwape nafasi viongozi wanaotokana na CCM" - Komredi Debora Joseph Tluway
Akiambatana na viongozi wengine UVCCM, Debora Joseph Tluway ametembelea Kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi Mangapwani. Pia, amezindua amsha amsha ya Upashikaji wa Bendera kwa Mabalozi; Ametembelea Bandari ya Mafuta Mangapwani
Vilevile, Debora Joseph Tluway amezindua Mashindano ya Vijana 50 ya Uendeshaji wa Baiskeli yanayoendelea katika Jimbo la Chaani na amempongeza Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mhe. Juma Usonge kwani amekuwa Kiongozi anayefikika, anasikiliza Vijana na anafanya kazi kwa vitendo.
Attachments
-
KKV.mp455 MB
-
BASKELI.mp479.6 MB
-
AMSHA.mp479 MB
-
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.27.jpeg264.7 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.26.jpeg306.1 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.30 (1).jpeg259.2 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.28 (1).jpeg220.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.30.jpeg303.5 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.29.jpeg245.3 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.36.jpeg274.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.25.33.jpeg278.6 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 21.16.02.jpeg144.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 21.16.10.jpeg125.7 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 21.16.17.jpeg245.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 21.16.19.jpeg222.2 KB · Views: 3