Decoder ni Kisimbuzi na sioi King'amuzi

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Posts
1,757
Reaction score
277
Leo BAKITA wameujulisha umma tafsiri sahihi ya maneno kama ifuatavyo:

Decoder............. Kisimbuzi (kusimbua -decode)

Detector........... King'amuzi (kung'amua - detect)
 
Leo BAKITA wameujulisha umma tafsiri sahihi ya maneno kama ifuatavyo:

Decoder............. Kisimbuzi (kusimbua -decode)

Detector........... King'amuzi (kung'amua - detect)

upo sahihi mkuu.
 
Sikubaliani na BAKITA wanaposema mfumo wa dijitali uwa mfumo wa dijiti au wa kidijiti.
Kwa maoni yangu uwe MFUMO WA TARAKIMU kwa vile digit = tarakimu.
 
Na receiver maana yake ni nini?
 
Sikubaliani na BAKITA wanaposema mfumo wa dijitali uwa mfumo wa dijiti au wa kidijiti.
Kwa maoni yangu uwe MFUMO WA TARAKIMU kwa vile digit = tarakimu.

Ila BAKITA wamekuwa ni kizingiti ktk ukuaji wa lugha
 
Sidhani kama tutaendelea kwa kutungia vitu walivyogundua wenzetu majina, mara mpakato, mara king'amuzi mara kisumbuzi, eeeh.

Kwanza lugha huwa haitungwi.
 
Sidhani kama tutaendelea kwa kutungia vitu walivyogundua wenzetu majina, mara mpakato, mara king'amuzi mara kisumbuzi, eeeh.

Kwanza lugha huwa haitungwi.

We kwa mawazo yako kukua kwa lugha kunakuwaje?
 
Sidhani kama tutaendelea kwa kutungia vitu walivyogundua wenzetu majina, mara mpakato, mara king'amuzi mara kisumbuzi, eeeh.

Kwanza lugha huwa haitungwi.

Km lilivyo vazi la kitaifa -- hili ndio limeniwacha hoi zaidi!!
 
Leo BAKITA wameujulisha umma tafsiri sahihi ya maneno kama ifuatavyo:

Decoder............. Kisimbuzi (kusimbua -decode)

Detector........... King'amuzi (kung'amua - detect)

Kwa mujibu wa mjadala ulioendeshwa kupitia radio 1 katika kipindi cha ulimwengu wa kiswahili, kinachurushwa kuanzia saa 1:30 asubuhi (MUHIMU: kipindi kilirushwa siku ya jumamosi ya tarehe 5/1/2013); DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.
Decode ni muunganiko wa maneno mawili, CODE na DE, na neno DE limetumika kama kikanushi/kinyume. Mfano: KWELI na SI KWELI. CODE linatafsirika kama SIMBA (sio simba mnyama) kwa lugha ya kiswahili. Na DECODE linatafsirika kama SIMBUA wa lugha ya kiswahili. SIMBA (sio simba mnyama) kinyume chake ni SIMBUA. Na kifaa kinachotumika kusimbua kinaitwa KISIMBUZI, yaani DECODER kwa kingereza.
Lakini neno DETECTOR tafsiri yake ni KING'AMUZI. Na ving'amuzi viko vya aina nyingi, mfano:
Metal, X-rays, Uranium, Gas, Moisture, Blood sugar na Bomb DETECTORS; yaani ving'amuzi vya kung'amua metali, miale ya X, madini ya Uranium, Gesi, Unyevu, sukari ya damu na mabomu.
Kumbuka DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…