Ded - aliyetoa machozi kishapu aagizwa na bosi wake!!!

SpK

Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
40
Reaction score
5
Bw. Mlaki ametakiwa kuheshimu mamlaka ya madiwani

2009-02-03 12:31:28
Na ITV Habari


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali mstaafu Dkt. Yohana Balele amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Bw. Jesse Mlaki kuheshimu mamlaka ya madiwani.

Dkt. Balele ametoa agizo hilo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kupata malalamiko kutoka miongoni mwa madiwani hao kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akikiuka utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya baraza lao.

Amesema madiwani ndiyo wawakilishi wa wananchi katika halmashauri hiyo hivyo mkurugenzi hana budi kuwaheshimu, kufanyia kazi na kutekeleza maamuzi yote ya vikao vyao ambapo pia amemtaka awe akiwapatia taarifa za fedha zinazoingia katika halmashauri hiyo kutoka serikalini na kuwasomea mapato na matumizi wanapoyahitaji.

SOURCE: ITV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…