DED anapo kataa kupitisha kibali cha uhamisho

DOMBWELA

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
757
Reaction score
843
Habari wanajamvi, inapotokea mtumishi amefuata taratibu zote za kuomba uhamisho, yaani ameomba nafasi ya kuhamia sehemu kupitia kwa mwajiri na akajibiwa kupitia kwa mwajiri kuwa nafasi ipo na baadaye mwajiri huyo akakuombea kibali Tamise kupitia kwa RAS, Katibu mkuu tamisemi anatoa kibali cha uhamisho wako na baadaye DED anakataa kupitisha kibali na kukufungia data sheet sababu eti hujakidhi vigezo. Wanaojua mniambie ikoje hapo, maana ndugu yangu yamempata hayo, anaomba ushauri na msaada afanyeje ili kuondokana na hilo!.
 
Toa Rushwa Ili Uhudumiwe,everyone Is Corrupt,even Our Country Is Corrupt so Let Us Be Corrupt!
 
Reactions: y-n
Huyo mpeleke takukuru,anataka rushwa.Atakufungia kwa lazima.Atakuwa acting DED nini!
 


Anakwambia hujakidhi vigezo VP???? Nakushauri ukatoe malalamiko Kwa RAS maana Tayari RAS Wa mkoa wako anayo nakala ya kibali hicho kilichotoka Tamisemi. pls lishughulikieni faster ndani ya siku 14.
 
Haiwezekani vinginevyo ndugu yako alijipitishia mwenyewe barua ya kuomba nafasi
 
Wadau wote nashukuruni kwa ushauri wenu mzuri mlionipa na kuendelea kunipa kwa njia mbalimbali umenifikia na utanifikia, ngoja niufanyie kazi.
 
Nawashauri wana jamvi msiwe wepesi wa kumtetea mtoa hoja kabla hajatoa maelezo ya kutosheleza...kuna uhamisho mwingi wa kimagumashi tamisemi...nitatoa mfano:
Kuna siku nilikuwa tamisemi dodoma ofisi za elimu, nikiwa humo ofisini alifika dseo wa Ileje na barua sita za uhamisho wa walimu wa wilaya hiyo kwenda maeneo mengine...
Dseo alileta zile barua ili ajue zimetolewa tolewaje wakati hao walimu hawakupitisha barua kwake/ded, walikuwa na kesi za kinidhamu...kumbuka barua za uhamisho zimetolewa na tamisemi...dseo alikomaa akitaka maelezo ya nani alitoa barua kwa niaba ya katibu mkuu...siku hiyo ile ofisi ilikuwa ndogo.
Kilichonifurahisha ni uungwana ulioonyeshwa na maafisa wale wa tamisemi kwani walikiri majina ya walioandika barua kwa niaba ya katibu mkuu ni ya wafanyakazi wa ofisi hiyo lakini sahihi hazikuwa zao...
Wakaamua kusitisha uhamisho wa walimu wanne kati yga sita...
Mtoa hoja eleza vizuri inawezekana kuna kanuni au taratibu umezikiuka, huenda hicho ndicho kinachompa jeuri ded wako kama alivyokuwa na jeuri dseo wa Ileje, jeuri ambayo nillipenda...

Tafakari...
 
Sema ni Halmashauri gani uambiwe kama huyo DED ni mwadilifu au la!
 
Ndg yangu unachosema nitofauti naninacho kiombea ushauri kutoka kwa wadau ili ndugu yangu huyo apate haki yake. Mimi ninachosema taratibu zote zilizingatiwa, DED kupitishia barua ya kuomba nafasi na nafisi ikapatikana, akamuombea kibali cha kuhama kupitia RAS, ndizo kumbukumbu zilizoko mikononi mwa huyo ndugu ambazo nami nimeziona.
 
Ndg yangu intonjanda unachosema ni tofauti unapotoa ushauri/msaada zingatia maelezo yangu ya awali niliyo tolea mada kuomba ushauri/msaada kwa wanajamvi, maana hayo ndiyo yenye ushahidi ambao na mimi kama mtu mzima ninayezingatia maadili, utaratibu, kanunu na sheria nimeuona mikononi mwa kijana.
 


Mkuu ndombwela, andiko langu lilikuwa na nia njema ili wadau wapate mahali pazuri pa kuanzia kutoa ushauri mujaarabu...
Nimezungumzia "barua za magumashi", viambatanisho vyote huwepo na wakati mwingine ndani ya ofisi kuna kuzungukana , kuna wakati maafisa utumishi wanasaini kwa niaba ya mkurugenzi, hapo ndipo tatizo linapoanzia...
Lakini labda niweke kile ninachokifahamu kuhusu uhamisho ndani ya tamisemi:
Hatua ya awali ya kuomba uhamisho, barua itaanza kusainiwa na kule anakotaka kuhamia ili kupata uthibisho kama nafasi ipo, itakuja kusainiwa pale anapotoka then katibu mkuu...
Inawezekana ndugu yako alipita hatua zote hizo bila ushikishwaji wa kikanuni wa mwajili wake (ded)...
Pia, naomba ieleweke kwamba ninaelewa fika wapo ma-ded wengine wana matatizo ya usumbufu usio wa lazima...
Nimeandika kwa kufupisha, nitashukuru kama utakuwa umenielewa...

Tafakari...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…