LGE2024 DED Kilosa: CHADEMA walikwamisha Uchaguzi Ruaha jana

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Imeelezwa kuwa sababu zilizopelekea kata ya Ruaha, jimbo la Mikumi, mkoani Morogoro yenye vijiji vinne (4) na vitongoji 21 kushindwa kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa hapo jana, Novemba 27.2024 badala yake kufanyika leo, Alhamisi Novemba 28.2024 ni kutokana na vurugu zilizoanzishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye eneo hilo

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Michael John Gwimile alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na Jambo TV leo ambapo amesema kuwa vifaa vya uchaguzi vilifika kwenye kata hiyo siku moja kabla kama ilivyokuwa kwenye maeneo mengine lakini tatizo lilianzia pale viongozi wa CHADEMA walipohitilafiana na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata hiyo kwani walijitokeza kudai kuwa vifaa hivyo havitoshelezi na hivyo kuzuia visisambazwe kwenye vituo husika hadi wavikague

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Amesema kwa mujibu wa taratibu vifaa vya uchaguzi vinapaswa kufunguliwa kwenye vituo husika ambapo kutokana na mazingira ya uchaguzi huo vituo vya uchaguzi vilikuwa ngazi ya vitongoji na vijiji hivyo kwa kuwa kila chama cha siasa kimeweka mawakala viongozi hao walielezwa kuwa mawakala wao kwenye vituo husika ndio wenye mamlaka ya kujiridhisha kuhusu vifaa hivyo na sio wao jambo ambalo inaonekana lilikuwa gumu kueleweka na viongozi hao wa CHADEMA

"Ushirikiano haukuwa mkubwa sana kwenye makubaliano na kwa bahati mbaya sana muda ule wa mwisho wa kufunga vituo vya uchaguzi ambao ni saa 10 ulikuwa umeshafika kwa hiyo ikabidi tuje tufanyanao vikao, Kamati ya Usalama ya wilaya ilikuja ikafanya vikao pale pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na mimi mwenyewe nilikuja nikafanyanao vikao baadaye tukafanya consultation na Wizara yaani TAMISEMI tukaona ni bora sasa kwa sababu muda umekwenda hatuwezi kufanya uchaguzi muda huu (yaani jana usiku), tukaona bora tufanye leo"

Amesema kanuni zinamruhusu msimamizi msaidizi wa uchaguzi anapokuwa amekutana na jambo lisilokuwa la kawaida atashauriana na msimamizi wa uchaguzi kuona namna ya kuhairisha uchaguzi kwenda siku nyingine
 
Kuhusu madai ya uwepo wa idadi kubwa ya maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama walioko kwenye vituo vya kupigia kura leo, Mkurugenzi huyo amesema naye amepokea malalamiko hayo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, lakini alichowajibu ni kwamba kutokana na kile kilichotokea jana ambacho kwa kiasi kikubwa kingeweza kuhatarisha usalama, kinachofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama ni sehemu ya tahadhari tu hivyo wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi wowote badala yake wajitokeze kwenda kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka

"Mimi pia nilienda pale jana, na nilienda kwa lengo la kukutananao ili tujadiliane namna bora ya kutatua hili jambo kwa njia ya amani, lakini wao walikuwa wamekusanya watu wao (wanachama/ wafuasi wa CHADEMA), kwa hiyo mimi nilivyofika pale nilikuta kundi kubwa linazomea lakini sisi tukaona tuvumilie tu ili tutafute njia ya kutatua hiyo shida kwa sababu lengo letu sisi ni uchaguzi ufanyike kwa uhuru na amani" -DED Kilosa

Awali akizungumza na Jambo TV leo, Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mikumi Ally Rashidi alidai kuwa uchaguzi huo ulishindwa kufanyika hapo jana kutokana na uwepo wa vifaa vichache vya kupigia kura jambo ambalo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa amelikanusha, kwa kile alichoeleza kuwa Halmashauri hiyo ina kata 40 lakini ni kata hiyo pekee ambayo haikufanya uchaguzi hapo jana.
 
Back
Top Bottom