Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wakulima wa zao la Ngano Wilayani Makete, wameshauriwa kutumia Mashine bora za kisasa katika Uvunaji wa zao hilo, ambao umeshanza rasmi katika baadhi ya Maeneo ikiwemo kijiji Cha Mlengu kilichopo Kata ya Kigala.
Ushauri huo umetolewa Julai 13, 2024, na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Samwel Sweda, wakati wameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, katika Ukaguzi wa shughuli za Uvunaji wa zao hilo katika mashamba hayo yenye ukubwa wa zaidi ya Ekari mia tatu.
Ikumbukwe kuwa, ni wiki Moja tu imepita tangu Mkurugenzi huyo, wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, alipotembelea mashamba hayo, ambapo aliwataka wakulima hao kuwa na Imani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwakuwa soko la zao hilo lipo Kwa asilimia miamoja kupitia Kampuni ya Bakhiresa iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Uvunaji wa zao la Ngano, umeanza rasmi Julai 13, 2024, katika Mashamba hayo yaliyopo kijiji cha Mlengu, Kata ya Kigala, Wilaya ya Makete, mkoani Njombe.