DED Sumbawanga amtimua fundi kutokana na ubabaishaji usiozingatia viwango vya ujenzi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi. Pendo Mangali katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo aliyoifanya Februari 22/2025, ameagiza kuondolewa kazini kwa fundi Yusuph Benias Mgogo na kutafutwa fundi mwingine kutokana na fundi huyo kuwa mbabaishaji na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ubora na viwango vinavyostahili.

Bw. Mgogo ambaye alikuwa akihusika katika ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Sumbawanga pamoja na ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi katika kituo cha afya Senga alibainika kutozingatia viwango vya ujenzi, ramani na michoro aliyopewa na Serikali na hivyo kuharibu miradi.

Vilevile fundi huyo ameonyesha kukosa uwezo wa kitaalamu wa ujenzi licha ya kuwa na vyeti vya taaluma hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi. Pendo amesema Halmashauri haiwezi kumvumilia fundi kanjanja ambaye anatumia fursa za kuomba kazi kwenye mfumo wa NesT ilhali hana ujuzi wa kazi za ujenzi na kutaka kuja kujifunza kujenga kwenye miradi ya Serikali.

Akizungumza baada ya kuondolewa kwenye kazi hiyo Bw. Mgogo alikiri kuwa hana ujuzi wa kutosha katika fani ya ujenzi na kuomba huruma ya Mkurugenzi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi. Pendo Mangali katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo aliyoifanya Februari 22/2025, ameagiza kuondolewa kazini kwa fundi Bw. Yusuph Benias Mgogo na kutafutwa fundi mwingine kutokana na fundi huyo kuwa mbabaishaji na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ubora na viwango vinavyostahili.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…