DED wa Bagamoyo atoa fursa ya uwekezaj katika ufugaji wa jongoo bahari

DED wa Bagamoyo atoa fursa ya uwekezaj katika ufugaji wa jongoo bahari

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
NJOONI MUWEKEZE UFUGAJI WA MAJONGOO - DED BAGAMOYO

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda, ametoa fursa kwa wawekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kuja kuwekeza katika ufugaji wa Majongoo bahari.

Wito huo ameutoa Juni 20 mwaka huu wakati akizungumza na madiwani na wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha walipotembelea wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya uendeshaji wa Halmashauri za wilaya nchi.

Amesema Bagamoyo kuna fursa nyingi za uwekezaji ambazo hutumii mtaji mkubwa ambapo mtu au taasisi ikiamua kuja kuwekeza wilayani Bagamoyo basi pesa ipo nje nje.

"Bagamoyo kwa kuwa tuna bahari yenye uwanda mkubwa inafaa sana kwa kuwekeza kwa kilimo cha mwani na ufugaji wa majongoo bahari ambayo kwa sasa soko lake lipo juu sana" amesema Mkurugenzi Selenda.

Amedai kuwa kwa soko la sasa kilo moja ya majongoo bahari inaanzia Tsh. 170,000 mpaka 180,000 hivyo ni fursa ambayo ni ya uwekezaji usiohitaji mtu au taasisi kuwa na mtaji mkubwa wa fedha.

Pia, Mkurugenzi huyo amesema Wilaya yake ya Bagamoyo ina maeneo makubwa ambayo yanafaa pia kwa kilimo cha miwa ambapo bado wakulima wadogo wadogo wanahitajika kulima zao hilo na kuliuza kwenye kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo.

Madiwani wa halmashauri ya wilaya kibaha wamesifu uendeshaji mikutano kisasa kwa kutumia vishikwambi na masuala mengine ya kiutawala ambayo yanaendeshwa na halmashauri ya wilaya bagamoyo ambapo wamesema wamejifunza mengi ikiwemo masuala ya utalii, kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini ya kujengea (mchanga).

Madiwani hao na baadhi ya wakuu wa idara walipata fursa ya kutembelea soko kuu la Samaki Bagamoyo kwa kujifunza mapato yanavyokusanywa, matumizi ya nishati safi kwa kukaangia samaki pamoja na kuona vivutio vya kitalii pamoja na sehemu ambazo panachimbwa madini ya kujengea (mchanga).

20240621_152106_InSave_0.jpg
20240621_152106_InSave_1.jpg
20240621_152106_InSave_2.jpg
20240621_152106_InSave_3.jpg
20240621_152106_InSave_4.jpg
 
Back
Top Bottom