Defao aonekana Nairobi akiwa kachoka!

Ubavu

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
2,790
Reaction score
3,263
Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa, na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.

Defao ambaye hata hivyo haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka huko Kenya, kutokana na muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri kuyumba kisanaa na kiafya kwa msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa yake katika bara la Afrika na Ulaya.

Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.


 

Mungu wangu huyu mgonjwa huyu
 
Wababa wengine..Mungu awasaidie tu...hivi akijiangalia kwenye kioo anajiona yuko sawa tu...anyways...acha niheshimu machaguzi yake...

Defao ni baba jina...!
 
Duuuh...sijawahi muona ya zamani...embu wekeni tuone
 
Mbona kama katuni vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…