Defensive Driving

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
8,130
Reaction score
8,362
Andika chochote ukijuacho kuhusu defensive driving.

Mimi naanza na hii;
1. Fanya ukaguzi wa gari kabla hujaanza safari yeyote.
2. Heshimu speed limit.
3. Ata kama ni haki yako kupita jiridhishe kwanza kabla haujapita hasa maeneo ya junction na kwenye taa au mzunguko (round about).
4. Usiendeshe ukiwa umelewa
5. Macho yako yawe yaconcentrate barabarani na kwenye vioo (side mirrors, hind mirrors) na gari za mbele na pembeni (blind sports) na si chura za wanawake.
6. Hakikisha unaacha umbali wa kutosha baina yako na gari la mbele
7. Epuka destructions zozote wakati unaendesha kama simu, maongezi n.k akili yako iwe barabarani.
8.
9...
10
 
7. Funga mkanda uingiapo kwenye gari.
8. Lock milango uingiapo kwenye gari.
9. Hakikisha seat ya dereva imelock kwenye reli zake uingiapo kwenye gari.
10. Usiendeshe na kutuma au kusoma message..
 
Mmmmh mkuu mita 2?!!...mbona naona kama ndogo sana... mita 2 kati ya gari na gari hapo sio defensive drive mkuu..hio itakuwa Attacking drive πŸ˜€
inatakiwa 2 -3 seconds not 2 miter..na unahesabu 1001, 1002 kutoka gari ya mbele inapopita stationary object na unapokifikia wewe
 
Mmmmh mkuu mita 2?!!...mbona naona kama ndogo sana... mita 2 kati ya gari na gari hapo sio defensive drive mkuu..hio itakuwa Attacking drive πŸ˜€
Kwa madereva wajuaji wa Dar, ukiacha hiyo mita 2, mtu anachomeka gari yake, ukiacha tatu anaona we ni learner.

Inawezekana, ila mara nyingi ukiwa kwenye High way, hasa unapokuwa nyuma ya malori......waendesha Auto hawawezi kukuelewa.
 
4: Acha mita 2 au zaidi kati ya gari yako na gari ya mwenzako
unapoendesha gari yako.
5: Sima ukatizapo kivuko cha waenda kwa miguu.
Hiyo namba 5 inatakiwa usimame tu au usimame kukiwa na mtu anataka kuvuka?
 
Hii ni ya muhimu lkn hamna aliyesema usiendeshe ukiwa umelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…