Defensive Driving

inatakiwa 2 -3 seconds not 2 miter..na unahesabu 1001, 1002 kutoka gari ya mbele inapopita stationary object na unapokifikia wewe
km ni Highway na ni speed zaidi ya 50km/h pori kwa pori hata hiyo meter 2 haitoshi
Sheria Mjini wanataka yard 10 au mita 2 au 3 lkm km ni foleni meter 1 tosha hakuna mtu atachomeka ila Breki uwe nazo si za kuchochea
 
Usiendeshe gari ukiwa na usingizi/shusha vioo ukiwa unasafiri usiku umbali mrefu usije ukasinzia.

Ukishindwa tafuta sehemu salama paki gari chapa usingizi dakika 20
 
Wakuu kuna hizi taa za LED zinamwanga mkali sana..yani deam light utafikiri mtu amewasha Full..mnawezaje kukabiliana nazo..na vipi ukikutana na mtu amewasha full huwa mnakabiliana naye vipi
 
Muhimu zaidi.

Lazima uwe na gari,usiendeshe mifuniko ya ndoo za maji barabara huku ukizingatia sharia zote za uendeshaji,wewe bado utakuwa ni dungaembe tu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
una mahusiano mazuri na ajali aiseeeee......[emoji45] [emoji45]
Weeeeh! Ile kitu inakatiza mbele ya car screen! Kitu mgongo binuka, chura wowowo, moja hamsini lingine mia, kifua kidogo na embe dodo zilizochongoka, bado ile mwendo yake ya kubembeleza afu kitu inatikisika mtindo wa kuita afu unazungumzia eti nisiangalie furaha ya macho. Hapo ajali wala haiwezi kuja bhana, nambie kitu ingine!
 
Ukiendesha barabarani ujue unaendesha magari matatu au zaidi; kwa hiyo unatakiwa ujitahidi kufuatilia mienendo na maamuzi ya dareva wa mbele yako na nyuma yako ili kusaidia kuepusha ajali. Utafanikisha haya kwa kuepuka na ushindani usio na maana na kufanya kila njia kuhakikisha kua wewe na majirani zako barabarani mnakuwa salama kutokana na maamuzi yako.
 

Natambua uwepo wa like ya Founder wa JF kwenye uzi huu
 
Pale taa ya kuruhusu-Kijani () inapowaka kuna umuhimu mkubwa sana wa kuacha sekunde mbili hadi tatu kabla hujakanyaga mafuta na kuingia barabarani au kuingia kwenye mzunguko.
Kwanini unatakiwa kufanya hivyo...
1. Si kila mmoja yupo makini barabarani kuna mwingine anakimbizana na taa hivyo inapowaka taa nyekundu upande wake anaweza shindwa simama kutokana na hilo mnaweza jikuta mmekutana kwenye mzunguko
2. Kuna wengine hawafahamu vizuri alama za taa za kuongozea magari..inaweza waka taa za kuruhusu magari yanayonyooka yeye akaingia na kukunja kushoto au kulia.
3. Kuna wengine huwa wanaconfuse kati ya taa ya njano na kijani huyu naye usipoacha muda wa kujiridhisha unaweza kutana naye katikati.
4. Kuna magari mengine mabovu au hayana breki taa inapowaka nyekundu upande wake au njano anaweza shindwa kusimama..sasa ww ukiingia mkuku mkuku mnaweza kutana kati kati..
5. Boda boda na bajaji hawa huwa hawaangalii ni taa zipi zimewaka...na zpi zimewaruhusu au kuwataka wasimame...hawa usipokuwa makini unawez Kutana nao katikati.
 
Usiendeshe gari yako tu ili kuepuka ajali bali endesha gari nne zinazokuzunguka au mbili kwa baadhi ya barabara. Gari nne iliyo mbele yako, nyuma yako na zile mbili za ubavuni kwako kulia na kushoto. Kwa maana hiyo macho yako yanatakiwa yafanye kazi ya ziada ili kuepuka ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…