Degree inagharimu si chini ya milioni 10, kwa hali ya ajira ya sasa siwezi kumsomesha mtu kozi zenye uhitaji mdogo, heri aende veta au nimpe mtaji

Degree inagharimu si chini ya milioni 10, kwa hali ya ajira ya sasa siwezi kumsomesha mtu kozi zenye uhitaji mdogo, heri aende veta au nimpe mtaji

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ni kweli kuna tatizo la ajira lakini viwango vimetofautiana kwa kozi

Kuna kozi kama Bima, Environment, Philosophy, siasa, Business administration, n.k. Ni ngumu kujiajiri na ni nadra kusikia tangazo la ajira.

Wakati huo kusomesha mtu degree bila mkopo kinahitajika kiasi cha milioni 10 kwa kujibana bana

Pocket Money miezi tisa kwa miaka mitatu
150,000*9*3 = 4,050,000

Ada - 1,500,000 *3=4,500,000
  • Hii ni ada ya chuo cha serikali nje ya kozi za science (computer, udaktari, engineering, n.k), vyuo private vina ada kubwa zaidi.

Hostel - 500,000*3=1,500,000

Jumla 10,050,000

Halafu mtu arudi mtaani mwaka mzima kuna matangazo mawili ya ajira 😑😓, kujiajiri hawezi 😔 kuna utofauti gani na kuzichoma milioni 10 kwenye tanuri la moto ?

Nikisikia "Baba / mjomba / Shemeji naomba unisomeshe degree ya siasa" sina huo uwezo, Ni heri uende veta kisha nikupe mtaji.
 
Tulimsomesha kijana mmoja Veta na mwingine degree ya education.Yule wa Veta ndani ya miaka miwili alifanya kazi za carpenter akasaidia nyumba ya baba yake ya matofali kijijini kwa asilimia %75 na sasa hivi wazazi wake wanalala huko.Ila huyu wa degree bado anajitolea na mizinga mingi.Sisemi degree ni mbaya ila kuna ambazo ni upotevu wa muda tu
 
Education ilikuwa enzi hizo kabla ya 2015, Yani ukimaliza degree yako serikali inakupangia shule fasta.

ajira za ualimu zimekuwa changamoto, kuna utitiri wa vyuo vya ualimu halafu mbaya zaidi hata wale waliosomea kozi nyingine sikuhizi wanaajiriwa kuwa walimu (fani imevamiwa).

Shule za private hali ni mbaya zaidi, wanafunzi wanalipa ada milioni 3 walimu wenye mikataba wanalipwa laki 3
 
Education ilikuwa enzi hizo kabla ya 2015, Yani ukimaliza degree yako serikali inakupangia shule fasta.

ajira za ualimu zimekuwa changamoto, Shule za private hali ni mbaya zaidi, wanafunzi wanalipa ada milioni 3 walimu wanalipwa laki 3
Kuna wanaolipwa hata sh laki mbili,hali ni mbaya sana
 
Somesheni watoto Open University, degree ya science unaimaliza kwa chini ya 3mil. Hapo mtoto yuko huru kitaa akifanya biashara zake.

Hii mm imenisave sana, na ajira nilipata taasisi x.

Open inaweza kuwa njia bora zaidi kwa baadhi ya watu hasa kama mtoto ana self discipline.
 
Back
Top Bottom