Dejan anavyoimarishwa

Vawulence

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
1,930
Reaction score
2,118
Baada ya mechi ya ngao ya jamii, watu wengi wamekuwa wakimshambulia mchezaji mpya wa Simba toka Serbia na kudai kuwa hana kiwango cha maana.

Wengi wamediriki kusema alikuja na mzigo wa jezi wa VB na Simba wakamsajili.

Wengi wa wanaomsakama Dejan ni washabiki wa Yanga.

Kwa upande mmoja wengi wa washabiki wa Simba wanachukulia kitendo hicho kama ni ubaguzi hasa wanaposikia akitaniwa kwa kuwa tu ni mzungu.

Jambo moja ni wazi kuwa kama masimango hayo yatachukuliwa vyema, basi ni njia nzuri ya kumjenga na kumuimarisha Dejan.

Kuna mifano mingi ya wachezaji waliopitia ubaguzi lakini wakafanya mambo makubwa... Kwa uchache niwataje Pele, Drogba, Okocha, Dani alves, Etoo na Thiery Henry.

Kwa sasa mashabiki wa Simba wawe watulivu wamuache Dejan aelekeze hasira anazopata kwa kubaguliwa na wanaUtopolo wakiongozwa na Zeruzeru wao.

Kuna siku wataimba nyimbo za kumsifu "mzungu"
 
Hakuna mwana simba anayekubali huo upuzi wa huyo mzungu,hanakiwango cha kucheza simba
 
Unamtoa Kagere ili umlete huyo mzungu. Kwamba ndo upgrade au? Kama si uzuzu ni nini?
 
Hivi unaelewa maana ya hilo neno ubaguzi mbona nyie majeneza fc mnapenda kukuza mambo anachofanyiwa huyo mzungu hakina tofauti na cha kina yikpe,molinga,kindoki mbona sisi hatukusema mnawafanyia ubaguzi huo ndyo utani.mnatafuta pa kutokea baada ya kuwafilimba kwa mkapa
 
mlete mdhungu aliyekuja na Vifaa vya Sensaaaa
 
Wewe ni JK ama Sunday Manara? Nimesema kuwa washabiki wa Simba "wanahisi" kuwa kitendo hicho ni ubaguzi.... Ajabu unanishambulia bila sababu.
 
Hakuna mwana simba anayekubali huo upuzi wa huyo mzungu,hanakiwango cha kucheza simba
Kwa hiyo wewe umeongea na wanasimba wote mkakubaliana kuwa mzungu hana kiwango?
 
Kupitia hili jukwaa nimegundua watu tusio na ajira ila tuna bando tupo wengi sana.

Yaani tunabishana vitu vya kijingajinga..
 
Dah ila watu!!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ko mzungu alikuja na marobota ya jezi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…