Dejavu, Titanic na CNN

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Umewahi kuwa kwenye mazingira au hali Fulani, alafu una ikimbuka kwa karibu asilimia 90, unahisi kama hiyo siku na wakati unajirudia, unaweza otea hata kitu kinacho fuata baada ya sekunde kadhaa na kinatokea kweli!

Kwa kiswahili ni kusema kuwa umesha ona hayo mazingira kabla , kingereza ni already see ila wa faransa wanaita De javu.

Sayansi, Dini na tamaduni, zinaelezea hii hali kwa namna tofauti tofauti.
-
November 19 mwaka 1938 Cincinnati Marekani alizaliwa bwana mmoja alie itwa Jina la Robert Edward Turner , ambae baadae alikuja kuanzisha kituo maarufu Dunia Cha habari CNN,

wakati CNN ikiwa kwenye hatua za mwanzo sana za ukuaji Robert aliwaagiza wafanyakazi wake kuwa anahitaji atengenezewe kwaya itakayo imba wimbo mzuri ambao chaneli yake ya CNN, inta ucheza wakati ambao Dunia itakua inaisha.

Yaani alitaka kwaya itakayo kuwa ikiimba kwenye chaneli yake ya CNN, wakati wa mwisho wa Dunia ,
Kwaya iliimbwa akiwa kama muongozaji wa kila kitu kianzia sauti mpaka video.

Miaka 12 baadae video hii ilikuja kuvuja na ikawa hadharani na walio ijua waliitazama (Ipo YouTube search doomsday CNN anthem) Utaipata)

-
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 na mwishoni mwa miaka ya 90 filamu maarufu na iliyo toa watu machozi walipo angilia, TITANIC.

hii filamu ilitoka miaka takribani 20 baada ya kitu cha habari cha CNN kuanzishwa na muasisi wake kutengenezea kwaya kwa ajiri ya mwisho wa Dunia. Katika hali isiyo ya kawaida kwenye filamu hii wakati meli inazama ilikuwepo kwaya ambayo yenyewe haikuacha kupiga mziki, licha ya kuwa kila mtu alihaha kunusuru uhai wake , kwaya Ile iliendelea kuimba mpaka mwisho wa meli kuzama hwakukoma.

Sasa, Ile kwaya iliyo pigwa kwenye Filamu ya TITANIC inafanana Melody na mashairi na kwaya Robert Edward.
-
Director wa wa filamu ya Titanic James Cameron ndio aliitaka scene hiyo na yeye ndio alie simamia kuanza uandishi na kila kitu alitaka kwaya iwe vile na ipige bila kukoma.wakati watu wakiangamia na kuhaha,

Kwenye mahojiano tofauti ya James Cameron director wa Titanic na Muasisi wa CNN ,Rober wote walisema kuwa walikua na maono ya kuwa siku ya watu kuangamia kutakua na kwaya inapiga bila kukoma kwaya ambayo inaimba vizuri sana ila inatisha lakini pia James Cameron Ali kiri kabisa kuwa hakua anaijua Ile kwaya ya CNN , sababu wakati huo haikua ime vuja hivyo kwaya Ile ni maoni yake kwa asilimia 100,

-
Dini ya watu wa India budha wanaamini kwenye kuzaliwa tena(The reincarnation) wanaamini kuwa kama mtu alifa leo basi roho/nafsi yake itahamishiwa kwa kiumbe mwingine hivyo Kuna wakati nafti hizo hukumbuka yake yalio jiri wakati huo wa uhai wa mwanzo , ndio maana mtu anajikuta ana pitia De javu ,

Wanasayansi wao wanasema kuwa ni ubongo tu Huwa una jaribu kuringanisha nyakati ambazo zinaendana ,

Wahenga wao wanasema ni mizimu inajaribu kukuambia kuwa , wako nawewe na wanakuonesha kuwa wanakujari ,

De javu ya James Cameron na Robert Edward Turner zinafanyanana kwa zaidi ya 90% ziki eleza jambo sawa,
Nimechagu kuchagu De javu ya wahenga.
 
Kwenye Theory ya Multiverse theory ya dunia kama hii kwenye ulimwengu yenye version yako wanasema kwamba deja vu huwa ni tukio alolifanya mtu kama wewe au version yako kwenye ulimwengu mwingine hivyo kuna muda universe zina link ndio una experience deja vu
 
Very true
 


Duh kumbe kuna mimi mwingine.
 
Wanadai Ulimwengu na viumbe vyote tupo katika Matrix na infinity vitu/muda na matukio tunayodhani yamepita au yanakuja kiuhalisia Haya exist ni illusion tu

Yaani kiufupi hatuelewi kama hatueleweki kumbe vitu tutakavyofanya future tulishafanya na tulivyofanya vilishafanyika kabla hatujafanya
WTF!

Time is illusion!
😁😁
 
Point to note

Wahenga wao wanasema ni mizimu inajaribu kukuambia kuwa , wako nawewe na wanakuonesha kuwa wanakujali
 
Kuna ndoto naota ilishajirudiaga zaidi ya mara kadhaa kwenye nyakati tofauti tofauti. Inaonesha nipo kwenye gari inaenda kasi sana inapotea njia tunaanza kuparamia miti ila nafanikiwa kujiokoa natokea mji flani ninavyoingia kwenye huo mji naanza kutembea kutafuta msaada nikawa naishia kati naamka ila ule mji nikawa hadi nimeukalili setting yake. Huwezi amini huku nilipo sasa nina mwaka naishi huku yani ni copy kabisa ya ule mji niliokuwa nauota na ile ile ndoto haijarudi tena. Huu mji nilipo sasa ni mkoa wa mbali ambao tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kufika...
 
"Nearer my God to thee"
 
Lakin vipi kuhusu kuona mazingira kama uliyo wai kuyaona yakihusisha technologia ya wakati huu mfano magari je aliewai kuexprience kitu kama hiki pia alikuwa kwenye ulimwengu wa tech za sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…