Democrat wamteua rasmi Joe Biden kuwa Mgombea Urais wa Marekani

Democrat wamteua rasmi Joe Biden kuwa Mgombea Urais wa Marekani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kitaifa wa Chama cha Democratic nchini Marekani wamemteua rasmi Joe Biden kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika baadae mwaka huu.

Marais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton na Jimmy Carter, walimpigia debe Biden kuwa mtu mwenye uzoefu na uadilifu wa kuinusuru Marekani iliyoathiriwa vibaya na janga la virusi vya korona. Kongamano hilo la siku nne, mwaka huu linafanyika kwa njia ya vidio kutokana na janga la COVID-19.

Katika ufunguzi wa mkutano huo mkuu uliofanyika kwa njia ya vidio, mke wa aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, Bibi Michelle Obama, alisema Rais Donald Trump wa chama cha Republican alipata muda wa kutosha kuthibitisha kuwa anaweza kufanya kazi ya kuliongoza taifa, lakini ameshindwa.

1597823103067.png
 
Back
Top Bottom