Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Democtratic, plutocracy vs meritocratic system, federal vs unitary state
1. Marekani na tanzania zote ni nchi za kidemokrasia. Lakini marekani ni #federal state, wakati tanzania ni #unitary state.
2. China na tanzania zote ni unitary state, lakini tanzania ni nchi ya kidemokrasia(democratic state) wakati china ni #meritocratic state.
3. Unitary state (unitary government) ni mfumo wa kiutawala ambao executive (serikali) ina nguvu kuliko mihimili mingine. Nchi ambayo viongozi wa chini wanatii amri(order) kutoka juu. Kwa lugha ya kingereza, #unitary state is the governing system in which the government (executive) has the #total power over all its other #political subdivisions (judiciary and parliament).
Ni nchi ambayo mamlaka ya rais ni makubwa sana, hayabishaniwi. Akiagiza, ameagiza na wale wa chini wanawajibika kutii. Hapa lazima utii chain of command. kwa hiyo kabla ya #kumlaumu rais kwamba anaingilia mihimili mingine, ni vema mfahamu kwamba, tanzania sio federal state, ni unitary state. Kuna wakati mnampa rais lawama asizostahili kutokana na uhaba wa maarifa. Kwa katiba ya tanzzania, rais ni mkuu wa nchi, mkuu wa mahakama(anamteua jaji mkuu), mkuu wa bunge(anamteua katibu wa bunge).
4. Federal state (usa) ni mfumo wa kiutawala ambao mihimili mikuu ya serikali inajitegemea. Bunge na mahakama zinafanya kazi kwa mujibu wa katiba, bila kupokea maelekezo yoyote kutoka serikalini.Kila muhimili unatekeleza majukumu kama yalivyoainishwa na katiba bila kupokea maelekezo kwa mtu au muhimili mwingine, hakuna kuingiliana. Marekani pia inaundwa na majimbo huru, yana viongozi wake wasiopokea maelekezo kwa raisi. Ukitumia demokrasia ya marekani kukosoa demokrasia ya tanzania unakosea, kwa sababu, marekani ni federal state, wakati tanzania ni unitary state.
5. Democratic state ni nchi ambayo, viongozi wake wanapatikana kwa njia ya kuchaguliwa, kupigiwa kura wakati meritocratic state (kama china) viongozi wake wanapatikana kwa njia ya promotion based on performance. #katika mfumo huu, #mafanikio ya mtu, #kupata kazi au #kupanda cheo kunatokana na #uwezo binafsi, #kipaji chake, #juhudi, #wingi wa maarifa.
Yaani ili upande cheo, lazima kwanza uwe bora na uoneshe sifa (potentials) fulani kwamba unavitu vya tofauti. Wewe ni bora na umesabaisha matokeo fulani fulani katika maeneo yako ya kiutendaji. Kutokana na mfumo huu(meritocratic system), huwezi kukuta viongozi vilaza au watendaji vilaza china. #mfumo huu umewafanya #wachina wafanye kazi kwa bidi na #wanasoma sana. Na hapa ndio utofauti wa china na Tanzania unapoanzia.
Na hii ni moja ya sababu, kwa nini wachina wanaweza kufanikisha ndoto yao ya kuitawala dunia. Jombaa, hawa jamaa wametengeneza mifumo imara isiyo na longolongo. Kama unaweza, unaweza tu na kama unastahili cheo au kazi utapata bila kulamba miguu ya mtu. Kama umetenda kosa na unatakiwa kufungwa, jombaa utafungwa tu, yaani hakuna wa kukusaidia, hakuna cha god father.
6. Aristocracy (aristocraric system) ni mfumo wa kiutawala ambao, watu hupata kazi, kupanda vyeo kutokana na #historia za baba zao, #vyeo vya baba zao, #hadhi ya familia zao. #hapa tanzania #inabidi tubadilike. Mfano ni nchi za kifalme, sasa tanzania tujitazame sana
7. Plutocracy ni mfumo wa kiutawala ambao watu wenye pesa(matajiri) wanatumia pesa zao kushinda chaguzi au kutawala. Jamii inayotawaliwa na watu wenye pesa au utajiri, wenye mali. Kwa kifupi, ili uwe kiongozi lazima uwe na pesa, mali, ukwasi. Tanzania ijitazame sana kwenye hili. Mnaweza kusema mna demokrasia kumbe ni plutocracy.
8. Ndugu zangu, kama tunataka kwenda #kwa kasi, #meritocratic system ni nzuri kuliko #democratic system. Licha ya ukongwe katika mfumo wa demokrasia, mpaka leo, demokrasia ya Marekani ina ujanja ujanja mwingi, rafu nyingi sana, matumizi ya pesa ni makubwa mno. Propaganda za hovyo kibao, matendo ya udhalilishaji wa utu wa mtu ni makubwa sana. Licha ya kuwa na mifumo imara, bado demokrasia ya marekani ina madhaifu mengi. Je, vipi kuhusu nchi changa kama tanzania? Vyanzo vya vurugu nyingi duniani ni demokrasia.
Mungu ibariki Tanzania.