Demokrasia: CCM itaacha lini utamaduni wa Rais kuwa Mwenyekiti wa Chama?

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,104
Reaction score
2,550
Kwa muda mrefu Chama cha Mapinduzi kimeendeleza utamaduni wake wa kuminya demokrasia ndani ya chama hicho kwa kuwanyima wanachama wake wanaotaka kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama Taifa na kulazimisha Rais aliyeko madarakani agombee nafasi hiyo kwa kupambana na 'kivuli'.

Mbaya zaidi wakati wa kuhesabu kura 'kivuli' hakina wakala wa kusimamia kura zake na kusababisha mawakala wa Rais kubadilisha kura za hapana kuwa za ndiyo hivyo Rais kupata 'ushindi'wa asilimia 100.

Ni lini CCM itaachana utamaduni huu wa kizamani na wa hovyo sana ili kulinda demokrasia ndani ya chama hicho?
 
Mbona mwandishi unaandika kama wewe si mwanachama wa chama hicho? Waachie mambo yao
 
Kwani katiba ya CCM inasemaje juu ya uenyekiti?
 
nitachagua kupata UHURU,HAKI NA MAENDELEO YA WATU kupitia CHADEMA.
Vipi huko kwenu, Mbowe apewe 20 mingine!
 
Je ni lini muheshimiwa mbowe atakoma uenyekiti wa Chadema?muhimiwa namuomba Mnyika niongozane naye ili anieleweshe zaidi naomba swala. Langu liingizwe kwenye ansadiii...asante muhishimiwa Mkuu..kama Bungen vile natania tu...sina chama mie,...Nakuchagua kutokana na kazi yako tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…