SoC01 Demokrasia huchochea mabadiliko katika jamii

SoC01 Demokrasia huchochea mabadiliko katika jamii

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 14, 2021
Posts
1
Reaction score
0
DEMOKRASIA

Ni aina ya utawala ambayomaamuzi huamuriwa na watu. Pia demokrasia huruhusu maamuzi mbalimbali kufanyika kupitia nguvu ya watu. Demokrasia huruhusu uhuru wa watu, vyama vingi vya siasa, uhuru wa vyombo vya habari na usawa katika sheria. Demokrasia huchochea mabadiriko katika jamii ni kama ifuatavyo;

Uhuru wa watu binafsi - Watu wanapokuwa huru kujishughulisha katika masuala mbali mbali ya kujenga kujijenga kiuchumi huweza kujipatia kipato kinachowezesha watu kujipatia maendeleo yao binafsi , jamii wanamoishi , wilaya , mkoa na taifa kwa ujumla.

Demokrasia huchochea mabadiriko kwa kufuata misingi ya demokrasia na kuwaruhusu watu kuwa huru kufanya shughuli zao kwa uhuru pasipo kubughudhiwa. Kuwa na sawa wa kijinsia,Katika jamii yetu tunapokuwa na usawa wakijinsia katika masuala yote yanayotujumuisha tukijenga utaratibu wa kuheshimu haki sawa kwa wote katika umilikaji wa rasilimali na mali za familia hutuwezesha kuondoa dhana potofu zinazoturudisha nyuma katika maendeleo. Jamii yetu ya kitanzania sehemu kubwa kuna ugandamizwaji wa usawa wa kijinsia hasa kwa wanawake hii hutokana na mila na desturi ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa na huchangia sana kudidimiza usawa katika jamii zetu.

Demokrasia huchochea mabadiliko haya kupitia vyombo vya habari, maandiko ya makala mbalimbali, sanaa na makusanyiko ya injili lengo likiwa katika kuelimishana ili jamii yetu iweze kutambua thamani ya utu wetu, maendeleo ya kila mmoja wetu na taifa.

Kufanya chaguzi huru na za haki - Katika chaguzi za viongozi hasa katika nchi yetu ya Tanzania tunahitaji kuwa na uchaguzi unaozingatia mapendekezo ya watu na maoni pia kuheshimu kura za watu wanazopiga.Demokrasia huchochea mabadiriko haya kuzingatia kanuni za uchaguzi tulizojiwekea lengo kupata viongozi waliochaguliwa kwa maoni ya wananchi na watakaofaa kutuongoza kwa muda wa miaka mitano.Kukosekana kwa demokrasia husababisha viongozi kuchaguliwa pasipo kustahili matokeo yake tunakosa maendeleo kutokana tu na viongozi hawana mitazamo ya kimkakati na wakati mwingine hawana sifa za kuwa viongozi.

Uhuru wa kutoa mawazo - Demokrasia huchochea uhuru wa watu katika kutoa maoni na mitazamo mbalimbali kijamii, kisiasa na kiuchumi. Watu wanaweza kutoa maoni na mitazamo yao kupitia mitandao ya jamii,mikutano ya hadhara na vipindi vya redio na Televisheni. Watuwanapotoa mawazo huweza kusaidia na kuwa mchango mkubwa wakuijenga nchi yetu hii inawezekana Iwapo Demokrasia ina mchango wake na kufuata kanuni na taratibu za kisheria pia kuzingatia katiba ya nchi.

Uwepo wa uwazi na uwajibikaji - Demokrasia huchochea mabadiriko makubwa katika uwazi na uwajibikaji. Watu wawekwe wazi na washirikishwe katika kuweka mipango ya maendeleo yao ndani ya jamii zao hii huweza kushiriki katika utunzi wa sera mbalimbali na sheria kwa kuzingatia uwazi pia kutoa mapato na matumizi katika ngazi za vijiji,mitaa, kata, tarafa,wilaya, mkoa hadi Taifa.

Utawala wa sheria - Demokrasia huchochea katika mabadiriko ya utawala unaofuta sheria.Utawala wa sheria ni nguzo muhimu sana kwani kwa kuzingatia sheria wananchi hawawezi kuonewa na kunyanyaswa pia husaidia wananchi kuweza kupata haki stahiki. Kwa viongozi utawala wa sheria huweza kuwazuia viongozi kutawala bila kufuata sheria.

Kwa kuzingatia katiba ya nchi utawala wa sheria huchochea uwazi, uwajibikaji,

Haki za Binadamu - Demokrasia huchochea katika mabadiriko ya haki za Binadamu kila Binadamu ana haki ya kuishi,kumiliki mali.kupata elimu, kuwa huru, usawa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kusikilizwa, haki ya kutobaguliwa, haki ya uhuru wa mawazo na haki ya kufanya kazi.Kunapotokea viashiria vya uvunjifu wa haki za Binadamu mfano mauaji ya mara kwa mara, utekaji, unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, uuzaji wa dawa za kulevya maana yake haki za Binadamu haziheshimiwi katika jamii hiyo.

Demokrasia huweza kurahisisha katika kutetea na kukemea ili yawepo mabadiliko na watu kuishi kwa kuheshimu haki za Binadamu kwa kutambua usawa wa watu wote katika jamii na usawa wa watu wote katika sheria hakuna Binadamu aliyebora kuliko mwenzake wote tuko sawa hivyo Binadamu tuishi kutokana na kufuta taratibu na sheria.

Uvumilivu wa kisiasa - Demokrasia huchochea pia katika uvumilivu wa kisiasa.Katika nchi zenye demokrasia wanachama wa vyama vya siasa wenye itikati tofauti huweza kushirikiana na kuitanguliza jamii yao kuwa chachu ya maendeleo pasipo kujali tofauti zao za kisiasa, maoni na mitazamo tofauti.

Wanasiasa wakomavu huweza kufanya hivi lengo likiwa tu si siasa bali kujenga jamii yao. Hivyo wakiishi kwenye jamii yao kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kujaliana wataweza kupanga mikakati ya pamoja ya kimaendeleo bila kuchukiana na kupigana. Demokrasia huweza kuchangia hii kwa maana Demokrasia huruhusu uwepo wa vyama vingi na ushindani wa hoja kwa wanasiasa ili kuijenga jamii katika maendeleo.

Ukweli na usikivu - Demokrasia huchochea pia katika mabadiriko kwenye ukweli na usikivu. Katika jamii yetu viongozi wetu wanapaswa kuwa wakweli,wawazi, na wasikivu.Katika utendaji kazi wa viongozi hupaswa kuzingatia haya kwani ndio njia mojawapo ya kurahisisha majukumu yake aliypoewa na wananchi kiongozi muongo,fisadi,mbadhirifu wa mali za umma ni mara nyingi huwaanaminya Demokrasia ili kukidhi mahitaji yake binafsi kwa kutoonesha uhalisia wa masuala mbalimbali na muhimu katika jamii kwa utaratibu huo kiongozi huweza kuongoza na kuishi kwa mtindo unaomfaa ikiwemo kujilimbikizia mali wakati huo kuna maeneo yanayo hitaji huduma za kijamii mfano shule, hospitali, maji na nishati ya umeme.

Utendaji wa haki - Demokrasia huchochea katika utoaji wa haki katika makundi mbalimbali katika jamii zetu. Watu huwachagua viongozi maana yake viongozi hupewa mamlaka ya kuongoza kupitia watu. Kiongozi anapaswa kuwa mwadilifu,mwenye akili timamu,mvumilivu, mwenye upendo kwa watu wote, mkweli na muwazi. Kiongozi hapaswi kujiona mwenye haki zaidi katika mamlaka yake na kuwapuuza watu anaowaongoza. Demokrasia humfanya kiongozi kusikiliza watu wake maoni yao na kuyafanyia kazi.Viongozi wamepewa mamlaka kwamujibu wa taratibu za kisheria ili kiongozi aongoze kwa kuzingatia sheria .

Kiongozi anapaswa kuimarisha utendaji wa haki akiwa yeye ni mfano wa kutoa haki, hii humuwezesha kuimaisha upendo, umoja na amani na kupitia upendo, umoja na amani kiongozi huweza kuepusha jamii yake na migawanyiko inayoweza kujitokeza katika jamii kutokana na itikadi za kisiasa, tofauti za imani na masuala ya kiuchumi.

Maridhiano, Katika uongozi unaozingatia misingi ya utawala bora - Demokrasia huchochea katika mawazo mbadala ili kupata muhafaka kwa masuala yanayoigusa jamii.Maridhiano ni muhimu sana hasa baina ya pande zinazokuwa mvutano kwa maslahi ya jamii.Maridhiano hayawezi kufanyika iwapo tu kutakuwa na viashiria vya kukosekana kwa Demokrasia ambayo huruhusu uhuru wa mawazo na uwepo wa vyama vingi. Kunapokuwepo na vyama vingi ni muhimu sana watu kuwa huru kujihusisha na masuala mbalimbali yatakayoweza kuwa mchango mkubwa kuijenga jamii.Maridhiano hufaa zaidi katika kuweka msingi wa umoja na mshikamano baina ya pande zenye mvutano pale tu kunapokosekana maelewano , umoja na mshikamano katika jamii.

Utungaji wa sera - Demokrasia huchochea mabadiriko katika utungaji wa sera ambayo wawakilishi wetu hupata fursa ya kutoa mapendekezo ambayo tunaweza kuyatumia kwa baadae kama sheria sera ni muhimu sana kutungwa katika mijadala ya wazi, upigwaji wa kura pamoja na kujumuisha vyombo vingine vya maamuzi mfano mahakama na makundi mbalimbali katika jamii.

Uboreshaji wa huduma za jamii - Demokrasia huchochea katika uboresha ji wa huduma za jamii katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kiulinzi na usalama. Ili tuweze kujenga uchumi imara hatuna budi kutengeneza mikakati ya ya kuweza kuinua uchumi wetu hivyo tunapaswa kuongeza nguvu kwenye Biashara, Kilimo ,ufugaji, uchimbaji wa madini,kuboresha utalii kwa kuongeza vivutio vyetu, kuwaandaa wataalamu katika vyuo vya ufundi pamoja na wazalishaji , kuwapatia mikopo makundi yote ya uzalishaji, kutoa semina mbalimbali za ufugaji wa tija , kulima kilimo chenye tija pia kuwatafutia masoko wazalishaji mali.

Kijamii tunahitaji kuwa na huduma bora za afya, huduma ya elimu, huduma ya kuboresha miundombinu mfano barabara na kuchimba mitaro ya kupitishia maji, huduma ya nishati ya umeme, huduma za maji na kuboresha mazingira kwa kupanda miti ya kutosha pia kuzuia shughuli za uhalibifu wa mazingira kwa mfano kuchoma mkaa na kukata miti ovyo. Kiutamaduni tunahitaji kuwa na uboreshaji mkubwa wa utamaduni kwa kuheshimu taratibu zetu, mila na desturi, miiko, mavazi, michezo ya kitamaduni mfano ngoma za makabila mbalimbali, nyimbo za makabila za asili yetu na kukemea mila na desturi potofu zisizokuwa na nafasi katika jamii ya sasa.

Ulinzi na usalama ni nguzo kubwa katika maisha yetu hivyo tusipokuwa salama hakuna suala lolote linaweza kutokea na Demokrasia haiwezi kuwepo endapo tu kutakosekana ulinzi na usalama serikali inahitaji kuwa na mkakati wa kuanzisha vikundi vidogo vidogo vya usalama ngazi za vijiji ,mitaa, kata, tarafa, wilaya , mkoa hadi taifa pia serikali inahitaji kuajiri wafanyakazi kwa ajili ya kuweka ulinzi na usalama katika maeneo yetu. Demokrasia inafanya kazi kubwa katika kuhamasisha masuala haya hasa katika kufanya maendeleo kwa jamii.

Tathmini - Demokrasia huchochea mabadiriko katika jamii tathmini ni mchakato wenye lengo la kuangalia utekelezaji ulifanyikaje na kama malengo hayakufikiwa uboreshwaji wake unapendekezwa upi pia na matokeo ya programu ambayo ni muhimu kuyatambua ili jamii iweze kupata maendeleo. Tathmini hufanywa na kila mmoja wetu ili kutambua malengo yetu iwapo yamefikiwa na kama malengo hayajafikiwa hatua za kufikia malengo huanza kuchukuliwa lengo ni kufikia malengo yetu tunayojiwekea haya yote hufanyika kwa kuzingatia misingi ya demokrasia inayojenga amani , upendo na mshikamano ili kuijenga jamii iliyo bora na yenye maendeleo.

Hivyo, Demokrasia ni msingi wa maendeleo kwa nchi yoyote ile Duniani na inapaswa kuheshimiwa watawala na Viongozi wetu.Vilevile Demokrasia ni nguzo muhimu kwani huwapa wananchi fursa ya kukosoa matumizi mabaya ya fedha, kusimamia miradi ya mendeleo katika jamii zao, kuhoji utendaji wa kazi katika ngazi za uwajibikaji,uwazi na uadilifu, kuunga mkono serikali kwa msauala mbalimbali yanayoigusa jamii ikiwa pamoja na kupeleka miradi ya maendeleo kwenye jamii zetu ambayo faida zake vijana hupata ajira na kujipatia kipato kinachowawezesha kukidhi mahitaji yao.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom