Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kinadharia Demokrasia ni Nguvu ya UMMA; ila kiuhalisia kuna utofauti mkubwa sana kutokana na ugumu katika utendaji au kwa ujanja na makusudi ya mifumo ambayo inanufaisha Status Quo
Je Demokrasia tunayotegemea imebakia kwenye Kuchagua watu wa Kutuamulia mambo au Kuchagua watu wa kuwakilisha mawazo yetu na kuweza kuwawajibisha wakati wowote wanapoenda kinyume ?
Je Demokrasia tunayotegemea ni ya kuchagua yule tunayemtaka wakati wowote au ni kubadilishana utawala kwamba kila mtu apate zamu yake ?
Ni wapi kuna umuhimu au ulazima wa kwamba mtu akitawala labda miungo miwili au mitatu basi awaachie wengine ? (Kama kweli UMMA una nguvu ya kuchagua kwanini wapangiwe muda wa kumchagua wanayemchagua) ? Na kuna nini huko hadi watu watake kwenda kama Nguvu ipo huku kwa Wachaguaji ?
Wazo Binafsi:
Nadhani tatizo kubwa ni Nguvu ya watawala (mtu anayechaguliwa) anakuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba ni vigumu kuwajibishwa na UMMA; Hivyo cha kufanya ni kumtoa Meno (Kumpunguzia Power) ili hata anapokuwa Kiongozi bado aweze kuwajibishwa / kukataliwa au hata kufukuzwa kirahisi wakati wowete ule, asiwe na nguvu ya kupanga (Mwenyewe) wala VETO yoyote, zaidi ya kuwa Symbolically..,
Tunaweza kujiona tumepiga hatua ila ukiangalia, hata Wafalme walikuwa wanachungwa na Miiko na Wasingeweza kufanya lolote... Pia tujiulize Je kama wananchi nguvu zetu zimebakia wakati wa uchaguzi (yaani kila miaka mitano au yoyote iliyopangwa) na Sio sisi tunaopanga vya kufanya bali tunapangiwa na tuliowachagua...., Je ndio hii Demokrasia tunayohitaji ?