JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ushirikishwaji wa Wananchi katika upangaji na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika Mtaa, hupelekea Wananchi kuwa na dhamana ya;
Kudhibiti Matumizi ya Rasilimali Katika Serikali za Mtaa kwa:-
➢ Kupitia vikao mbalimbali kama Viongozi na Wananchi wa kawaida.
➢ Kuhoji utendaji wa Viongozi wao kupitia vikao mbalimbali.
➢ Kwa kuwataka Viongozi wao kuwa wawazi juu ya mapato na matumizi na katika kuamua juu ya rasilimali mbalimbali za Mtaa.
Kuwadhibiti Viongozi wa Serikali za Mtaa kwa:-
➢ Kutochagua Viongozi wasio waadilifu na kuchagua Viongozi waadilifu.
➢ Kuwaondoa madarakani Viongozi wasio waadilifu kwa njia ya vikao halali kabla ya uchaguzi.
➢ Kuhoji utendaji wa Viongozi wao katika vikao mbalimbali vya kisheria wao wenyewe au kupitia wawakilishi wao.
➢ Kuhakikisha kuwa kuna uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali ya Mtaa.
Upvote
0