SoC03 Demokrasia na Utawala Bora katika Serikali Zanzibar

SoC03 Demokrasia na Utawala Bora katika Serikali Zanzibar

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
Joined
May 3, 2023
Posts
175
Reaction score
88
Katika shughuli za Serikali Zanzibar kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na Utawala bora kama ilivyoaiinishwa katika katiba ya nchi na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa wananchi; YAFUATAYO YAMEFANYIWA UTEKELEZAJI:-

1. Serikali imeanza kujenga jengo jipya la Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa na Uhujumu uchumi na kuipatia wataalamu na vifaa vya kisasa vya uchunguzi na kukamilisha uandaaji wa kanuni mbalimbali za udhibiti wa rushwa ,kwakuanzia mafunzo ya awali ya uchunguzi yalianza na wanafunzi 45 yalitolewa yaliyolenga kuwafanya watendaji kuwa wakakamavu katika kazi.

2. Skuli ya sheria Zanzibar imeanzishwa rasmi kupitia sheria Nambari13 ya mwaka 2019 na inaeendelea na kazi yake tokea uteuzi wa mkuu wa sheria Pamoja na wajumbe wa baraza la Skuli.

3. Mafunzo ya sheria kwa vitendo yametolewa kuanzia tarehe 17 Januari ,2022 ambapo mafunzo hayo yameendeshwa kwa awamu mbili Kwa miezi minne ya awamu ya awali wanafunzi wamepatiwa mafunzo ya sheria darasani na awamu ya pili wanafunzi wamepatiwa mafunzo hayo katika taasisi za serikali na binafsi.

4. Serikali ya Zanzibar imeweza kupitia na kuzifanyia marekebisho sheria zote zinazokwaza maendeleo ya kijamii na kiuchumi hususani sheria zinazozuia fursa za ajira kwa wananchi,Zaidi ya sheria 20 zimefanyiwa mapitio ,miongoni mwa sheria hizo ni SHERIA YA KUANZISHA OFISI YA MUFTI MKUU YA MWAKA 2021,SHERIA YA UTUMISHI WAUMMA NAMBA 2 YA 2011, WAKAGUZI WA HESABU,SHERIA YA UVUVI NAMBA 7 YA 2010,SHERIA YA ARDHI ENEO LA UTATUZI WA IGOGORO.KILIMO-SHERIA ZA MBEGU NA MINAZI,HUDUMA NDOGO ZA KIFEDHA,SHERIA YA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ,katika eneo la kikokotoo cha mafao ya wastaafu,sheria ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi ,Tume ya maadili ya uongozi wa umma,sheria ya Bohari ya madawa,Mfuko wa jimbo na Sheria ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali.

5. Baraza la wawakilishi limepitisha sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali na kuweka masharti bora ndani yake kama vile:-
a) Sheria ya kutoza kodi na kufuata baadhi ya kodi na Tozo na kurekebisha baadhi ya sheria za fedha na kodi zinazohusiana na ukusanyaji na udhibiti wa mapato ya serikalii na mambo mengine yanayohusiana na hay.
b) Sheria ya kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi (Appropriate bill)ya shilingi Trilioni 2.3
c) Sheria ya marekebisho ya sheria ya udhibiti wa Fedha haramu na mapato yatokannayo na uhalifu Namba 10 y mwaka 2009.
d) Sheria ya kuanzisha ofisi ya mufti mkuu wa Zanzibar na kuweka usimamizi bora wa shughuli za kiislamu Zanzibar na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

6. Kuimarisha mihimili ya mahakama na baraza la wawakiishi kwa kuwapatia rasilimali watu ,maeneo ya kazi na vitendea kazi,Utendaji wa mahakama umeendelea kuimarika kwa kuongeza idadi ya majaji ,Mahakimu na makadhi kutoka Majaji wanane 2021,hadi majaji 11 2022,wakiwemo majaji 4 wanawake ,mahakimu wa mikoa walifikia 30 2022 na makadhi wawili kwenye mahakama za kadhi.Mahakimu walifikia idadi ya 69 na makadhi 16 mwaka 2022.

7. Mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za udhalilishaji imefunguliwa rasmi katika mahakama za Mikoa Unguja na Pemba .Vilevile ,Mfumo wa uendeshaji kesi kwaw njia ya kielektroniki tayari umeandaliwa na kufanyiwa majaribio kwaajili ya kuendesha kasi ya uendeshaji wa kesi na mafunzo juu ya uingizaji wa kesi katika mfumo huo yametolewa kwa makarani wa mahakama kuu.

8. Vikao vinne mwaka 2022 vilfanyika vya kamati ya kusukuma mbele mashauri ya jinai vimefanyika,jumla ya kesi za jinai 5498 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali na kesi 3,482 zimetolewa uamuzi.

9. Jengo la mahakama kuu Tunguu limekamilika na linaendelea kufanya kazi.

10. Muhimili wa Baraza lla wawakilishi umeimarishwa kwa kupatiwa watendaji watatu kwa njia ya uhamisho,kununua vishkwambi zaidi ya 100 ,vipooza hew ana komputa.

11. Utekelezaji wa Sheria za Msaada wa kisheria ya Mwaka 2018 na Sheria ya Mawakili ya Mwaka 2020 ili kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote ,Mwaka 2022 jumla ya watoa huduma za msaada wa kisheria 214 wamesajiliwa upande wa unguja na Pemba na daftari la watooa huduma za msaaada lilitolewa kwa shehia 259.Nakala 250 za miongozo ya kuratibu huduma za kisheria ziligawiwa kwa serikali za mitaa ,nakala 400 ziligawiwa za muongozo wa upatkanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika vvyuo vya mafunzo na polisi ,nakala 400 ziligawiwa za muongozo wa upatikanaji wa sheria vizuizini.

12. Kulingana na ripoti ya mwaka 2022 taasisi zaidi ya 18 zilifuatiliwa zinazotoa huduma za msaada wa kisheria ,zaidi ya wananchi 2300 wamepatiwa elimu ya kisheria nan akala zaidi ya 350 za ripoti yam waka ya msaada wa kisheria yam waka 2019-2020 -2020-2021 zimechapishwa na kusambazwa na ripoti 125 za tathmini ya awali ya hali halisi ya msaada wa kisheria zimechapishwa na kusambazwa kwa wadau wa msaada wa kisheria .

13. Zanzibar imefanya ukaguzi katika wizara na taasisi zote za serikali ikiwemo ukaguzi wa Miradi inayosimamiwa na serikali Pamoja na Miradi inayosimamiwa na washirika wa maendeleo .Aidha ripoti ya ukaguzi imeendelewa kutolewa yenye viwango vya kitaifa na kimataifa kwa wakati.Ripoti za mwaka 2018-2019,ripoti za mwaka 2019-2020 na ripoti za mwaka 2020-2021 zote zimewasilishwa na zimekamilika na ziliwasilishwa barazani na kuendelea kufanyiwa kazi.

14. Wafanyakazi zaidi ya 40 wamepatiwa mafunzo ya Ukaguzi wa Hesabu unaozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ,mafunzo ya sheria ya manunuzi na TEHAMA.

15. Kongamano la kitaifa la utawala Bora lilifanyika tarehe 14/12/2022 katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil ambapo kongamano lilijumuisha watendaji wa ngazi mbalimbali serikalini ,katika kongamano hilo lilibainisha haja ya kupitia mapitio ya sera ya Utawala Bora yam waka 2012 nchini .

16. Kupitia vipindi vya redio elimu ya yraia na Utawala bora imeendelea kutolewa kupitia vipindi vya redio 80.

17. Elimu imeendelea kutolewa kwa Masheha na Madiwani katika wilaya 11 na miongoi mwa mada zilizowasilishwa na kujadiliwa ni Umuhimu wa kuzingatia maadili Pamoja na ujazaji wa fomu ya tamko la Rasilimali na Madeni ya viongozi wa Umma

18. Katika kuimarisha mfumo wa taarifa ,hadi mwaka 2022 serikali imesajili taarifa za viongozi wa Umma 2,415 katika mfumo wa kielektroniki na viongozi zaidi ya 80 wamehakikiwa taarifa zao za mali na madeni

MWISHO
Sote tujifunze kupitia kauli mbiu ya siku ya maadili na haki za binadamu ya 29/12/2020 liyosema,”TUIMARISHE UTOAJI WA HUDUMA KW KUZINGATIA MAADILI,KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU NA KUPAMBAA NA RUSHWA.”
 
Upvote 1
Back
Top Bottom