Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
DEMOKRASIA NA NCHI MASIKINI
Leo nakuja tena na hii mada.
Kwanza ijulikane kuwa hakuna nchi masikini imewahi endelea ikIwa chini ya demokrasia. Ukifutilia historia utaona kuwa hakuna nchi imewahi kutoka kwenye umaskini ikiwa inaongozwa kidemokrasia. Nchi zote zilizofanikiwa kutoka kwenye umaskini zimeongozwa kidikteta au kifalme.
Demokrasia ni anasa ya matajiri. Nchi masikini ikiingia kwenye demokrasia inajichimbia kaburi. Kwanza sababu ni kuwa ni gharama kubwa sana kuendesha nchi ya kidemokrasia. Nchi ya kidemokrasia ina walaji wengi sana.
Msomi mmoja alisema kuwa tofauti kubwa ya udikteta na demokrasia ni idadi ya watu unaotakiwa kuwaridhisha ili uendelee kushika madaraka. Idadi hiyo ni kubwa sana kwenye demokrasia. Wanaridhishwa kwa kupewa vyeo vingi vilivyoundwa kwa ajili yao. Na mzigo wote wa kuwalipa na kuwagharamia unaangukia nchi ambayo ni maskini.
Serikali ya kidemokrasia haiwezi kuja na sera za maendeleo ambazo zitawataka wananchi wafunge mikanda. Kuna wakati ili nchi iendelee ni lazima watu wafunge mikanda. Mfano nchi inaweza kusema hatutaagiza ngano ila tutahakikisha tunazalisha wenyewe kiasi cha kututosha. Kwenye nchi ya kifalme au kidikteta hilo linaweza kufanyika na baada ya muda nchi ikajitosheleza kwa ngano. Kwenye nchi ya kidemokrasia ngano ikiadimika wiki tu watu watangia barabarani na kuiangusha serikali. Wapinzani watapiga kelele za ajabu. Rais mwenye maono wa Liberia aliangushwa kwa namna hii na nchi ikachukuliwa na watu wazembe kama Samuel Doe. Ukisema tukuze textile industry yetu hivyo tulinde soko letu watu watazama barabarani na kukunyofoa madarakani. Waliotuletea demokrasia walijua vema wanachokifanya.
Kwenye nchi ya kidemokrasia ajenda kuu ya mtawala ni namna ya kubaki madarakani. Maamuzi yake yote yanazingatia kutimizwa kwa ajenda hii, hata kama yapo kinyume na maslahi ya nchi. Mfalme au dikteta anakuwa yupo imara madarakani. Anaweza kuwaza namna ya kukuza uchumi na hivyo kujiongezea kipato.
Nchi kama S Korea, Singapore, Malaysia na Shelisheli zimeweza kutoka kwenye umaskini kupitia madikteta.
Nchi kama UAE, KSA na Brunei zimeweza kufanya vizuri chini ya Ufame.
Bado hakuna nchi ya kidemokrasia iliyojitoa kwenye umaskini. Kila aina ya utawala ina mapungufu yake lakini demokrasia ni mfumo wa hovyo zaidi.
Habari kubwa kwenye nchi za kidemokrasia si za maendeleo, bali habari kuhusu michakato ya kidemokrasia.
DEMOKRASIA NA NCHI ZILIZOENDELEA
Nchi iliyoendelea na inayofuata demokrasia lazima itarudi kwenye umaskini. Nchi ya kidemokrasia iliyoendelea lazima itageuka ya kisocialist. Yaani wananchi wake watakuwa wanadai huduma kutoka kwa serikali kila leo hadi serikali itashindwa kuhudumia. Wananchi watataka afya bure. Mwanasiasa atakaye waahidi hilo wanamchagua. Kesho watadai elimu bure, kesho kutwa mishahara mikubwa, ruzuku wakulima nk nk. Nchi hizi zinajikuta zina matumizi makubwa kuliko mapato. Na wakati huo huo wanachi wakiwachagua wanasiasa wanaowaahidi kodi ndogo. Mwisho zinajikuta zina madeni wasiyoyaweza na deficit(nakisi) kwenye bajeti. Kaangalie nchi zinazodaiwa madeni ya kutisha, utakuta nchi za kidemokrasia zilizoendelea hasa ndizo zinaongoza kwa madeni, wala si nchi maskini zinazotangazwa kila leo. US deni lake ni asilimia 90 ya GDP yake. UK ni kama asilimia 250 wakati China ni kama 13%.
Hili la nchi kushindwa kumudu gharama limetokea kwa Argentina na nchi nyingi zilizoendelea zinaenda muelekeo huo.
Wafanyakazi wa nchi zilizoendelea na zinazofuata demokrasia wanaunda unions, na kudai mishahara mikubwa, benefits na haki nyingi. Matokeo yake gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa na nchi kushindwa kushindana na bidhaa za kutoka mataifa mengine kama China. Matokeo yake viwanda vinafunga.
Gharama za kujenga miundombinu kwenye nchi za kidemokrasia ni kubwa sana. China imeziacha mbali sana nchi za magharibi kwenye suala la treni ziendazo kasi. Sababu kubwa ni mchakato mgumu na gharama kubwa za kufanya hivyo kwenye nchi za kidemokrasia. Kwenye nchi za kidemokrasia ukitaka kujenga kitu utakutana na red tapes za maana. Kila kikundi kitatoa sauti zao. Wenye ardhi watagoma reli isipite kwenye mapori yao au watadai fidia za ajabu na kukupeleka mahakamani juu.
Wengi wape lakini wakati mwingine wengi hukosea vibaya sana. Suala la Brexit ni mfano wa hili. Watu wengi walipiga kura UK ijiondoe EU. Leo hii baada ya athari kubwa za Brexit waingereza wengi wanajuta na kusema kuwa suala la Brexit halikuwa sawa. Mambo ya kitaalamu hayapaswi kuendeshwa kidemokrasia.
Demokrasia haifai kwa nchi maskini. Tukae chini tutafute mfumo mwingine.