Nkuruma wa Karne ya 21
Member
- Jul 22, 2021
- 7
- 5
Na Nkuruma wa Karne ya 21.
Utawala bora unaoheshimu haki, Uhuru wa wote, haki sawa na furaha kwa wote hutokana na siasa safi inayosimamiwa na jamii chini ya mifumo Safi ya kisheria kupitia katiba iliyoandaliwa kwa ushiriki wa jamii husika.
Ni wazi kuwa kila binadamu anatamani kuiona jamii ikiishi katika Namna hiyo, na hili halipingwi kwa misingi ya Chama, dini Wala mihemko ya mtu kwa maslahi yake. Kila mtu anatamani Sana kuishi na kuona jamii ikiishi katika amani, furaha, haki na kushikamana vema huku ikisonga mbele katika ujenzi wa nyenzo muhimu za mahitaji ya maisha yao kama njia za uchukuzi, elimu, maji, afya na umeme.
Ili hayo yajengwe vema, jamii inahitaji katiba Safi inayotaja wazi Uhuru wa watu, haki za watu, utawala wa kisheria na misingi ya kidemokrasia kwa ujumla.
Rais wa zamani wa Marekani, Abraham Lincoln aliamini kuwa ili jamii iishi kwa furaha, amani na upendo na iweze kuendelea na kuishi kwa haki na usawa inahitaji serikali safi iliyotokana na jamii na itimize majukumu yake kwa kufuata matakwa ya jamii husika. Serikali ya kidemokrasia inatakiwa kutokana na watu na watawala waongoze watu kwa kuwarahisishia Upatikanaji wa mahitaji yao na si wachache kupeana fursa za uongozi wa jamii nzima na wachache hao kujipa nafasi ya kuamua maisha ya jamii nzima.
"Demokrasia ni mfumo wa serikali ya watu, inayotokana na watu kwa aili ya watu hao" ni kauli aliyoitoa Rais huyo wa 16 wa Taifa la Marekani ambapo alisisitiza kuwa Msingi mkubwa wa serikali ya kidemokrasia ni watu.
Watu wa jamii husika ndio wanaotakiwa kuwa na mamlaka, miongoni mwao watokee wagombea wa nafasi za uongozi zinazohitajika, na jamii yao ichague wale wanaowataka na watakaochaguliwa waongeze kwa maslahi na matakwa ya jamii hiyo.
Kinachoumiza jamii nyingi duniani ni pale ambapo maneno ya falsafa hii yanaishi vinywani mwa wanaotafuta fursa za uongozi tu na wanapokuwa wameupata kwa kujiona hawawezi kuajibishwa aidha kutokana na mapungufu ya katiba za nchi zao wanageuka na kuanza kuwa watawala wa mambo yao (wabinafsi).
Si ajabu Sana hasa katika jamii za Afrika, hili lipo Sana, mtu anayesimama na kujinadi kuwa mtetezi wa wenye uhitaji, anatambua madhaifu yote yakisheria na anasimama kudai marekebisho lakini pindi atakapokuwa mamlakani tu ndio unakuwa mwisho wa madai hayo, anaenda kuungana na wale aliokuwa akiwalalamikia kuwa hawatendi sawasawa naye anaanza kutenda kama na pengine zaidi ya pale wanapoishia wao katika yale aliyosimama kuyapinga awali hadi akaaminiwa kupewa nafasi hiyo ili akayatekeleze.
Mwalimu JK. Nyerere katika moja ya nukuu zake muhimu aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Jamii ndiyo yenye wajibu wa kuwadhibiti viongozi wao na viongozi wanao wajibu wa kuheshimu haki za watu.
"Jamii inatakiwa kutokuwaogopa watawala, iwakosoe kwani jamii mkiwa waoga mtazalisha watawala madikteta" alisema Mwalimu Nyerere huku kuwaonya watawala wenye tabia za kuoneaonea watu, kupuuza puuza watu na kulazimisha yale wanayoyaamini waliopo madakani pekee kuwa ndiyo mawazo sahihi.
Wanaharakati wengi hasa Afrika na katika baadhi ya mataifa ya Asia na yale yenye tawala za kifalme huko Ulaya yamekuwa yakipuuza Sana Demokrasia kwa kuendelea na katiba zisizoendana na matakwa ya jamii, tawala za kurithishana yaani kizazi kilichotoa kiongozi mwanzoni mwa ujenzi wa mifumo kinadumu mamlakani vizazi na vizazi bila kujali uwezo na wingi wa rasilimali watu waliopo katika Taifa husika. Inakera sana.
Katika suala la utendaji wa haki katika mamlaka za utawala, kusimamia matakwa ya jamii nje ya matakwa ya wenye mamlaka, kuheshimu haki za binadamu, watawala wengi wamefeli Sana.
Wengi wamekuwa watam Sana mioyoni mwa watu katika Siku zao za awali madarakani kutokana na kauli zao zenye matumaini lakini Siku chache Sana baada ya kuanza kuongoza wamejikuta wakipoteza wafuasi wengi na kukimbilia kufunga ndoa na vyombo vya dola ili kuilinda tawala zao watimize matakwa yao ambayo mimsingi hata wao wanakuwa wanajua kuwa ikibiti mipango yao ipigiwe kura ya wengi kamwe haiwezi kukubalika.
Watawala wengi wenye sifa hizi huwa wanaamini kuwa kwa kutumia polisi wenye bunduki kutisha watu, magereza kuwaumiza wakosoaji wenye wafuasi wengi na mamlaka za mapato kiwatengenezea kashifa na kesi za kukwepa Kodi na kuhujumu uchumi huamini kuwa watadhaifisha upinzani ili dili zao waweze kuzipiga bila vikwazo na kushinikiza matakwa yao kwa nguvu watu watake wasitake yawezekane.
Kwa bahati mbaya Sana huwa wanashindwa kuuamini ukweli uliowazi kuwa upinzani si mtu Wala si watu, upinzani ni roho itokanayo na kutokuridhishwa na mifumo ama matendo yanayofanyika katika jamii.
Hivyo, kumuua mpinzani hata kuwafunga gerezani wote wanaoonesha mawazo kinzani na mfumo uliopo bila kuzishughulikia kero ama madai wanayoyasimamia hakujawahi kumaliza upinzani mahali popote duniani.
Wakosoaji wanaosimama na kusema hadharani wanakuwa kama mitume tu wateule wa Mungu ambao wanatumika kufikisha ujumbe wa wengi wanaosononeka mioyoni na wasiweze kusema, kumbe njia sahihi ya kumaliza upinzani ni kumaliza masuala yanayoibuliwa.
'Amani ni tunda la haki na bunduki ni silaha ya kupigana Vita vya silaha' falsafa hii ni muhimu Sana wote wanaopata neema ya kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kuziongoza jamii za watu kwani bila haki hakuna amani bali kutumia bunduki hulazimisha bunduki isiepukike kumaliza tatizo husika.
Maneno matakatifu kutoka katika Vitabu vitakatifu vyote, Kur'ani tukufu na Biblia Takatifu yanaeleza kuwa Mwanadamu si mkamilifu Bali Mungu pekee ndiye amekamilika.
Kwa kutambua ukuu huu wa Mungu Ni vema jamii ikatambua kuwa, kuwa na cheo fulani hakumfanyi mtu kuwa na akili kuliko wasio na cheo hicho na vivyo hivyo kuwa kiongozi hakumaanishi mawazo yako pekee ndiyo yanatakiwa kuamua nchi ama jamii iishi je, Bali kwa kuheshimu sheria za jamii husika (katiba), kutii na kutimiza mahitaji ya watu unaowaongoza na kusimamia misingi ya haki na juhudi zenye lengo la kupunguza kero za watu na kurahisisha maisha yao ni tunu pekee ambayo mwanasiasa ama mtawala anaweza kushinda hila zote na mapambano dhidi ya wakosoaji wake na si Yale maguvu, makaripio na matumizi ya magereza, vipigo na kuteka na kutesa wakosoaji kama ambavyo watawala wengi wasio na ujuzi wa mashauri ya jamii wamekuwa wakiamini na kutenda na kujikuta wakiongoza kwa misukosuko zaidi na kusahaulika Mara moja pindi wanapomaliza muda wao wa kuhudumu mamlakani. Viongozi andikeni 'Legacy' kwa wema, ubabe na kulazimisha matakwa yenu binafsi si dili.
0689990248

Upvote
0