Demokrasia ni mfumo mzuri ila una changamoto kubwa

Demokrasia ni mfumo mzuri ila una changamoto kubwa

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Demokrasia ni mfumo mzuri ila una changamoto kubwa bila jamii yenye
. Uelewa mkubwa katika mambo ya kijamii
. Uelewa mkubwa katika mambo ya kisiasa
. Kiwango cha juu cha ustaarabu

Demokrasia unakuwa mfumo mbaya katika jamii husika, kama unavyo fahamu kuwa demokrasia ni mfumo unaotoa kiwango cha juu kabisa cha uhuru hii ni hatari ukitumika katika jamii dhaifu.

Si ajabu kwenye demokrasia mtu mchekeshaji wa mitandaoni au mtu maarufu mtandaoni kuwania uongozi hata mkubwa wa Urais.

Demokrasia ni mfumo usio na mchakato mgumu sana wa kutwaa madaraka ukikubalika tu na watu hata kundi kubwa la wajinga tayari unautwaa uongozi.

Demokrasia ni mfumo unao hitaji umakini kuliko kuupaparikia.

Kiongozi anaeamuriwa na kundi dogo la wataalam walio na uelewa mkubwa wa masuala ya kuongoza hawezi fanana kamwe na kiongozi anaye chaguliwa na kundi kubwa la wananchi wajinga wanao rubuniwa na vitu vidogo vidogo kama umaarufu na kelele za majukwaani na wasio na ufahamu wa masuala mapana ya kidunia.
 
Back
Top Bottom